Pata taarifa kuu
TANZANIA-TETEMEKO

Tetemeko la ardhi laua Watu 11 na kujeruhi zaidi ya mia Tanzania

Watu kumi na mmoja wamepoteza maisha na wengine mia moja na sitini na mbili kujeruhiwa kaskazini magharibi mwa Tanzania baada ya tetemeko la ardhi lenye kipimo cha richa 5.7 kupiga mkoa wa Kagera,jeshi la polisi limethibitisha.

Harakati za kutathimini uharibifu zinafanyika na taarifa itatolewa lakini Kwa sasa hali ya utulivu imerejea
Harakati za kutathimini uharibifu zinafanyika na taarifa itatolewa lakini Kwa sasa hali ya utulivu imerejea RFI
Matangazo ya kibiashara

Kamanda wa polisi mkoani kagera Augustino Olomi ameiambia rfikiswahili kuwa harakati za kutathimini uharibifu zinafanyika na taarifa itatolewa lakini Kwa sasa hali ya utulivu imerejea.

Shakiru Hassan mkazi wa Muleba mkoani Kagera aliiambia Rfikiswahili kuwa maeneo yalioathirika zaidi mkoani humo ni Kitongoji cha Migala, ambapo baadhi ya nyumba zimebomoka na kupata nyufa.

Duru zinasema tetemeko hilo limeukumba pia mji wa Kampala na Rakai nchini Uganda saa 9 alasiri.

Mitetemeko mingine midogo pia ilisikika katika mataifa jirani ya Kenya Rwanda na Uganda.

Ripoti za kitaalamu zinadai tetemeko hilo limetokea katika mpaka wa Tanzania na Uganda, kilometa 47 kaskazini mwa Bukoba mkoani Kagera kufuatia mpasuko wa ardhi katika Bonde la Ufa la magharibi karibu kabisa na Ziwa Victoria.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.