Pata taarifa kuu
TANZANIA

Wahisani wajitokeza kuwasaidia waathiriwa wa tetemeko la ardhi nchini Tanzania

Wahisani mbalimbali wakiwemo Mabalozi wa nchi za kigeni wameahidi kusaidia kujenga upya makaazi na miundo mbinu muhimu iliyoharibika kama shule nchini Tanzania baada ya kutokea kwa tetemeko la ardhi mwishoni mwa wiki iliyopita mjini Bukoba Magharibi mwa nchi hiyo.

Jengo lililoporomoka mjini Bukomba nchini Tanzania baada ya tetemeko la ardhi
Jengo lililoporomoka mjini Bukomba nchini Tanzania baada ya tetemeko la ardhi cdn.guardian.ng
Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya Shilingi za Tanzania Bilioni 1 zimeahidiwa katika mkutano kati ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na wahisani hao wakiwemo wafanyibiashara waliokutana siku ya Jumanne jijini Dar es salaam.

Tetemeko hilo la ardhi ndio janga baya zaidi kuwahi kuikumba nchi hiyo ya Afrika Mashariki katika siku za hivi karibuni.

Idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na tetemeko hilo la ardhi lenye ukubwa wa ritcha 6, imefikia watu 17 huku mamia wakiendelea kupewa matibabu.

Siku ya Jumatatu, rais wa nchi jrani ya Kenya Uhuru Kenyatta, alitangaza kuwa serikali yake inatoa  msaada wa mabati, magodoro na vifaa vingine vya ujenzi kuwasaidia waathiriwa tetemeko hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.