Pata taarifa kuu
EAC

Viongozi wa EAC wakubaliana kuhusu mkataba wa kibiashara na EU

Viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wamekubaliana kuahirisha kwa miezi mitatu utiaji saini wa mkataba wa kibiashara kati ya Jumuiya hiyo na Umoja wa Ulaya.

Bendera za mataifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki
Bendera za mataifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki somalilandsun.com
Matangazo ya kibiashara

Umoja wa Ulaya ulikuwa umetoa hadi tarehe 1 mwezi Oktoba kwa Jumuiya hiyo kutia saini mkataba huo la sivyo, bidhaa kutoka mataifa hayo itozwe ushuru.

Mkataba huu utawezesha bidhaa kutoka mataifa ya EAC kutotozwa ushuru katika soko la Ulaya ilimradi tu ziwe katika hali nzuri.

Kuelekea katika mkutano huu, tayari Kenya na Rwanda zilikuwa zimetia saini mkataba huo, huku Uganda ikionesha nia ya kutia saini.

Tanzania kwa upande wake ilikuwa na mashaka kutokana na Uingereza kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya na kutoutia saini.

Burundi nayo ilisema iliukataa mkataba huo kwa sababu Umoja wa Ulaya umeiwekea vikwazo kutokana na mzozo wake wa kisiasa.

Akizungumza katika mkutano wa marais hao uliomalizika jijini Dar es salaam siku ya Alhamisi, rais wa Uganda Yoweri Museveni alisema kulikuwa na umuhimu wa mkataba huo kupitiwa upya na kuiomba Umoja wa Ulaya kutoiadhibu Kenya kwa kuzuia bidhaa zake au kuwalipiza kodi kubwa.

Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo na rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli amesema viongozi hao watakutana tena mwezi Januari kujadili suala hili kwa kina.

Naibu rais wa Kenya William Ruto kwa upande wake, amesema wamekubaliana kuwa mkataba huo wa kibiashara utapitiwa upya ili ukubaliwe kwa pamoja kama Jumuiya ya Afrika Mashariki.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.