Pata taarifa kuu

Kenya: Utata waibuka kuhusu fedha zilizotangazwa kuzuia athari ya El Nino

Kenya imekuwa ikikumbwa na mvua kubwa kwa siku kumi. Mvua zilizosababisha mafuriko makubwa, hasa katika maeneo ya pwani ya mashariki mwa nchi. Serikali ilitangaza kutolewa kwa shilingi bilioni kadhaa ili kukabiliana na athari za mfumo wa hali ya hewa El Niño. Lakini magavana wa mikoa iliyoathiriwa wanadai kuwa hawajapokea pesa hizi.

Abiria wakivuka maji baada ya kuhamishwa kutoka kwa basi la usafiri wa umma, kufuatia mvua kubwa iliyonyesha wilayani Kisauni, Mombasa, Kenya Novemba 17, 2023.
Abiria wakivuka maji baada ya kuhamishwa kutoka kwa basi la usafiri wa umma, kufuatia mvua kubwa iliyonyesha wilayani Kisauni, Mombasa, Kenya Novemba 17, 2023. REUTERS - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Nairobi, Gaëlle Laleix

Nchini Kenya, suala la fedha zilizotengwa kwa ajili ya kuzuia El Niño limezua utata. Kwa takriban siku kumi, nchi imekuwa ikikumbwa na mvua kubwa ambayo imesababisha mafuriko makubwa, hasa katika mikoa ya pwani ya mashariki mwa nchi.

Mnamo mwezi Septemba, serikali ilitangaza kuwa shilingi bilioni 10, au karibu euro milioni 60, zitatolewa ili kukabiliana na athari ya mfumo wa hali hii ya hewa. Lakini magavana wa mikoa iliyoathiriwa wanapinga hili.

Pambano hili linachezwa kupitia mikutano ya waandishi wa habari. Tarehe 22 Novemba 2023, baraza la magavana lilithibitisha kuwa halijapokea hata shilingi moja ili kukabiliana na mfumo wa hali ya hewa El Niño.

Jibu la makamo wa rais, Rigathi Gachagua, halikuchelewa kufika: “Tunashangaa kusikia magavana wakilalamika kutopokea pesa za El Niño kutoka kwa serikali. Magavana wanatarajiwa kutumia pesa za dharura kutoka kwa masharti yao ya kifedha na kutenga pesa kutoka kwa bajeti zao ili kuingilia kati. Serikali, kwa upande wake, imetoa shilingi bilioni 2.5 [takriban euro milioni 15] na itaendelea kutoa ufadhili katika siku zijazo. "

Baraza la magavana linabaini kwamba serikali inadaiwa na kaunti mbalimbali shilingi bilioni 62.5, au takriban euro milioni 375, kwa bajeti ya kawaida ya miezi ya Septemba hadi Novemba.

Ahmed Abdullah, gavana wa Kaunti ya Wajir, kaskazini-mashariki mwa nchi, anasema: “Hadi leo, hakuna kaunti ambayo imepokea pesa za kukabiliana na athari ya El Niño. Magavana wasiogope. Wanapaswa kuungwa mkono. Hawapaswi kugombana na watu au dhidi ya kila mmoja wao. Magavana hawako katika ushindani. "

Kulingana na mamlaka, mafuriko tayari yamesababisha vifo vya watu karibu hamsini na kuathiri karibu nyumba 80,000.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.