Pata taarifa kuu

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Kenya afariki katika ajali ya helikopta ya jeshi

Helikopta ya kijeshi ya Kenya iliyokuwa imembeba Mkuu wa Majeshi Francis Ogolla imeanguka katika mpaka wa Kaben-Cheptule kati ya Elgeyo Marakwet na Kaunti ya Pokot Magharibi katika eneo la magharibi nchini humo, takriban kilomita 400 kaskazini magharibi mwa mji mkuu Nairobi.

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF), Jenerali Francis Ogolla mnamo Septemba 21, 2023.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF), Jenerali Francis Ogolla mnamo Septemba 21, 2023. © Chief of the Kenya Defence Forces / twitter
Matangazo ya kibiashara

Ogolla amefariki baada ya helikopta aliyokuwa akisafiria pamoja na maafisa wengine kuanguka Kaben, Marakwet Mashariki siku ya Alhamisi.

Rais William Ruto ametangaza kifo cha Ogolla pamoja na maafisa wengine 9 wa jeshi huku wawili wakinusuruka.

Taarifa za awali zilizotolewa na chanzo kimoja cha polisi kilichozungumza kwa sharti la kutotajwa jina, askari watano wamefariki papo hapo na wengine watatu wamenusurika wakati ndege hiyo ilipoanguka, kulingana na shirika la habari la REUTERS.

Helikopta hiyo ya jeshi la Anga la Kenya aina ya Huey ilikuwa imetoka katika shule moja ya msingi ya eneo hilo ilipoanguka na kuwaka moto.

Msemaji wa serikali ya Kenya Isaac Mwaura kupitia mtandao wakijamii wa X, amesema kwamba taarifa rasmi kuhusu ajali hiyo itatolewa hivi karibuni.

Ogolla, 61, aliteuliwa kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Ruto Aprili mwaka jana. Ruto aliwaambia waandishi wa habari mwezi Mei mwaka jana kwamba alimteua Ogolla licha ya yeye kuwa miongoni mwa waliojaribu kubatilisha ushindi wake mdogo wa uchaguzi dhidi ya kiongozi wa upinzani Raila Odinga mwaka wa 2022.

Siku tatu za maombolezo ya kitaifa

Akitangaza kifo cha Jenerali Ogolla rais Ruto amesema kutakuwa na siku tatu za maombolezo kuanzia Ijumaa tarehe 19 Aprili ambapo bendera zitapeperushwa nusu mlingoti kwa kipindi hicho .

Amemtaja Jenerali Ogolla kama afisa shupavu aliyefariki akiwa kazini.

Maafisa hao walikuwa wamesafiri hadi eneo la kaskazini mwa Kenya ambalo limekuwa likikumbwa na visa vya wizi wa mifugo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.