Pata taarifa kuu

Kenya: Waliovuruga mikutano ya rais Ruto kuwajibishwa

Nairobi – Mamlaka nchini Kenya imeanzisha oparesheni kuwasaka watu waliovurugu mkutano wa rais William Ruto wikendi iliopita katika eneo la mkoa wa bonde la ufaa.

Rais William Ruto aliwakashifu viongozi wanaowachochea wapiga kura kutokana na tofauti zao za kisiasa.
Rais William Ruto aliwakashifu viongozi wanaowachochea wapiga kura kutokana na tofauti zao za kisiasa. © REUTERS/Michele Tantussi
Matangazo ya kibiashara

Kundi la watu katika kaunti za Bomet na Kericho walivuruga mikutano ya hadhara iliokuwa inaoongozwa na mkuu wa nchi kwa kupiga kelele.

Rais Ruto alikuwa katika eneo la mkoa wa bonde la ufaa ngome yake ya kisiasa kuzindua miradi ya kimaendeleo wakati mikutano yake ilipovurugwa na raia wanaoegemea mirango tofauti ya wanasiasa kwenye eneo hilo.

Suala hilo lilionekana kumkera mkuu wa nchi ambapo alitoa wito wa kukamatwa kwa viongozi wanaochochea vurugu kama hizo, hatua aliosema inatatiza miradi ya maendeleo.

Kutokana na agizo hilo, waziri wa usalama wa ndani Kithure Kindiki amewaagiza maofisa wa polisi kuwasaka waliohusika na kupanga na kuchochea matukio hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.