Pata taarifa kuu

Chama cha Bobi Wine chawasilisha kesi mahakamani kuhusu wafuasi wake

Nairobi – Chama cha National Unity Platform (NUP) nchini Uganda, kimewasilisha kesi mahakamani jijini Kampala kikiwataka maofisa wa usalama kuwaachia huru wafuasi wake 18 ambao hawajulikani walipo kwa kipindi cha miaka mwili sasa.

Bobi Wine- Mwanasiasa wa upinzani nchini Uganda
Bobi Wine- Mwanasiasa wa upinzani nchini Uganda REUTERS - ABUBAKER LUBOWA
Matangazo ya kibiashara

Wafuasi hao waliripotiwa kutoeka wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa 2021, uchaguzi ambao kiongozi wa chama cha NUP Robert Kyagulanyi Ssentamu, maarufu kama Bobi Wine, aliwania urais.

Licha ya wafuasi hao wa upinzani kutojulikana walipo, chama cha Bobi Wine na watu wa karibu wa wafuasi hao, wanasema wanaamini kuwa wanazuiliwa na maofisa wa usalama.

Hatua hii inakuja baada ya mwezi Oktoba mwaka uliopita, shirika la kutetea haki za binadamu nchini Uganda kumaliza uchunguzi katika kesi ya wafuasi hao, shirika hilo likisema kwamba halikuweza kuwapata watu hao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.