Pata taarifa kuu

Uviko: Uganda kuharibu chanjo zenye thamani ya euro milioni 6.7

Mamlaka ya Uganda itaharibu dozi milioni 5.6 za chanjo ambazo muda wake wa matumizi umekwisha dhidi ya Uviko-19, kwa thamani inayokadiriwa ya euro milioni 6.7, kulingana na ripoti iliyowasilishwa bungeni ambayo shirika la habari la AFP limepata kopi siku ya Jumatano.

Mkurugenzi mkuu wa Bohari ya Kitaifa ya Dawa (NMS), Moses Kamabare, ameliambia shirika la habari la AFP siku ya Jumatano kwamba mamlaka "hivi karibuni itashiriki katika uharibifu wa chanjo ambazo muda wake wa matumizi umekwisha."
Mkurugenzi mkuu wa Bohari ya Kitaifa ya Dawa (NMS), Moses Kamabare, ameliambia shirika la habari la AFP siku ya Jumatano kwamba mamlaka "hivi karibuni itashiriki katika uharibifu wa chanjo ambazo muda wake wa matumizi umekwisha." (c) Epicentre
Matangazo ya kibiashara

Chanjo hizi ziliagizwa na nchi hii ya Afrika Mashariki kama sehemu ya mkopo kutoka Benki ya Dunia.

"Kati ya dozi 12,595,920 za chanjo za Uviko-19 zilizopo, dozi 5,619,120 zimeisha muda wake. Thamani ya chanjo za Uviko-19 zilizokwisha muda wake kufikia tarehe ya ripoti ilikuwa shilingi bilioni 28.159 za Uganda", au takriban euro milioni 6.7, ameandika Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali John Muwanga katika ripoti yake ya mwaka ya fedha ya 2023 iliyowasilishwa bungeni siku ya Jumanne.

Mkurugenzi mkuu wa Bohari ya Kitaifa ya Dawa (NMS), Moses Kamabare, ameliambia shirika la habari la AFP siku ya Jumatano kwamba mamlaka "hivi karibuni itashiriki katika uharibifu wa chanjo zilizoisha muda wake".

"Hatujapokea maagizo ya chanjo ya Uviko-19 hivi majuzi. Ikiwa hakuna mahitaji kutoka kwa vituo vya huduma ya afya, tunatarajia chanjo zaidi kuisha (. ..) na kwa bahati mbaya hii inahusisha kiasi kikubwa cha pesa," amebainisha. Ripoti hiyo inahakikisha kwamba "fedha zilipatikana kutoka kwa Gavi (Muungano wa Chanjo, ushirikiano wa sekta ya umma na binafsi unaokusudiwa kuboresha ufikiaji wa chanjo katika nchi zisizo na uwezo) kwa kurejesha chanjo zote za Uviko-19 zilizoisha muda wake na uharibifu ".

Waziri wa Afya, Jane Ruth Aceng, aliliambia bunge mwezi Oktoba kwamba asilimia 59 ya watu wanaostahiki wamechanjwa kikamilifu dhidi ya Uviko-19. Uganda imerekodi rasmi visa 170,775 vya maambukizi ya virusi vya Corona na vifo 3,632 tangu kuzuka kwa janga hilo mnamo mwaka 2020, kulingana na data kutoka kwa Wizara ya Afya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.