Pata taarifa kuu

Vijana wengi Burundi watoroka nchi yao kwenda Serbia kutokana na hali ngumu ya maisha

Raia wa Burundi hasa vijana sasa, wameendelea kutafuta makazi mapya barani Ulaya kwa kusafiri kupitia nchi ya Serbia ambayo háina masharti magumu, wakiwa na lengo la kufika katika nchi za Umoja wa Ulaya kutafuta ajira, kufuatia hali ngumu ya kiuchumi katika nchi yao.

Uwanja wa ndege wa kimataifa Melchior Ndadaye, Bujumbura.
Uwanja wa ndege wa kimataifa Melchior Ndadaye, Bujumbura. Wikimedias
Matangazo ya kibiashara

Unapofika kwenye ofisi ya Ethiopian Air Lines jijini Bujumbura unakuta umati wa watu ambao wanatafuta tiketi ya kwenda Serbia. Raia hawa hawakubali kuongea na wanahabari. Lakini, mwandishi wetu mjini Bujumbura Jildas Yihundimpundu amebahatika kuongea na Evrard Nyandwi, kijana mmoja ambaye tangu wiki kadhaa anafanya biashara ili kutafuta nauli.

Ili mtu afike Serbia anahitaji kiasi cha pesa miliyoni 15 sarafu ya Burundi. Mimi sijapata pesa hiyo. Ndiyo maana kwa sasa ninajihusisha na bishara ya vocha hapa jijini. Nikieneza pesa hii, nitashika ndege moja kwa moja kwenda Serbia, hapa hali ya maisha ni ngumu. 

Ukosefu wa ajira, kukata tamaa katika maisha, ni miongoni mwa sababu zinazowafanya vijana wengi waondoke nchini Burundi. Lakini Serbia imekuwa njia tu ya kuwafikisha katika eneo la Schengen. Kukwepa polisi, wanatembea kwa miguu wakipita mabonde na misitu, amesema Prime Mbarubukeye, mkuu wa asasi huru inayopambana dhidi ya uhamiaji usio salama (ONLCT). 

Tarehe 23 septemba pekee, warundi wapatao 200 ndio walisafiri kwenda Serbia. Wote hao walibebwa na shirika la ndege Ethiopian Air Lines.  

Mwaka 2018, Burundi ilibatilisha utambuzi wa uhuru wa Kosovo. Kudhihirisha kuridhika kwake, Serbia iliwaruhusu warundi kuingia nchini mwake bila kuomba visa. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.