Pata taarifa kuu
DRC- BURUNDI-USALAMA

Burundi iliwatuma kisiri wanajeshi nchini DR Congo: Makundi ya kiraia

Burundi imetuma kwa siri mamia ya wanajeshi wake na kundi la vijana la Imbonerakure nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, tangu mwishoni mwa mwaka 2021 kupambana na kundi la waasi la RED-Tabara.

Vijana wa chama tawala cha Cndd-Fdd Imbonerakure,nchini Burundi
Vijana wa chama tawala cha Cndd-Fdd Imbonerakure,nchini Burundi Desire Nimubona/IRIN/www.irinnews.org
Matangazo ya kibiashara

Ripoti ya kundi moja la Haki za Binadamu nchini Burundi, Burundi Human Rights Initiative limesema lengo la serikali ya Bujumbura kutuma vikosi hivyo ni kupambana  na RED Tabara, ambalo serikali imesema ni kundi la kigaidi.

Hili limebainika licha ya serikali ya Burundi, mara kadhaa kukanusha madai ya kufanya operesheni za kisiri nchini DRC dhidi ya kundi hilo na badala yake kusema, vikosi vyake vinashirikiana vile vya Afrika Mashariki na Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa, kuleta amani Mashariki mwa nchi hiyo jirani.

Kwa zaidi ya miaka 10 sasa, wanajeshi wa Burundi na kundi la Imbonerakure, wamekuwa wakiwasaka makundi pinzani dhidi ya serikali, yanayoishi nchini DRC.

Tangu mwezi Desemba mwaka uliopita, ripoti ya Tume hiyo ya Haki za binadamu inaeleza kuwa wanajeshi zaidi ya 700 wamevuka mpaka na kuingia nchini DRC, huku wale wanaorejea nyumbani wakionywa kutosema chochote kuhusu operesheni hiyo.

Mwezi Mei, rais Evariste Ndayishimiye alisema yuko tayari kwa ajili ya mazungumzo na makundi ya waasi hasa REDTabara na NFL ambayo yamekuwa yakidaiwa kutekeleza mashambulio nchini Burundi tangu mwaka 2015.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.