Pata taarifa kuu

Uhaba wamafuta waendelea kutatiza shughuli Burundi

Kwa majuma kadhaa sasa nchi ya Burundi inashuhudia uhaba mkubwa wa mafuta ambao ulijotokeza nchini humo tangu mwezi Mei mwaka huu.

Katika picha baadhi ya waendesha bodaboda nchini Burundi, wakiwa na mitungi ya mafuta ya pikipiki zao kuelekea kutafuta bidhaa hiyo.
Katika picha baadhi ya waendesha bodaboda nchini Burundi, wakiwa na mitungi ya mafuta ya pikipiki zao kuelekea kutafuta bidhaa hiyo. © FMM-RFI
Matangazo ya kibiashara

Katika jiji la kiuchumi Bujumbura, kunashuhudiwa misururu mirefu ya magari na pikipiki mbele ya vituo vya kuuza mafuta.

Kwa miezi sita, hali imekuwa mbaya zaidi kwa waendesha boda boda ambao waliwekewa marufuku ya kuendesha vyombo vyao katikati ya mji.

Kinachofanyika wanalazimika kubeba mikononi matangi ya vyombo vyao ili wajaziwe mafuta.

Mwandishi wetu wa Burundi, Gildas Yihundimpundu alitembelea kituo kimoja cha mafuta katika jiji la Bujumbura.    

Usafirishaji wa abiria kwa njia ya bodaboda, ni biashara maarufu kwa vijana wanaotafuta ajira.

Kwenye kituo kimoja cha mafuta ambacho hatutakitaja jina, kuna matangi mengi ya pikipiki yenye rangi nyekundu, yakiwa yamewekwa chini, kwenye mstari. 

Mmoja kati ya waendesha pikipiki anasema ni kwanini wanafanya hivi. 

Tangu serikali iziwekee bodaboda marufuku ya kuingia jijini kati, tunalazimika kuondoa matangi kwenye pikipiki zetu, tunayabeba mikononi na kutembea kwa miguu tukitafuta mafuta. Hali ni mbaya ! Tukiyapata, tunashika Basi, tunarudi kule tulikoacha pikipiki ili tuzirejeshee yale matangi   
Baadhi ya waendesha bodaboda wakijadiliana jambo wakiwa na mitungi ya pikipiki zao.
Baadhi ya waendesha bodaboda wakijadiliana jambo wakiwa na mitungi ya pikipiki zao. © FMM-RFI

Emmanuel ni mwendesha bodaboda amepiga foleni kwa muda wa saa 8 akitarajia kupata lita 10 za kuweka katika tangi lake.

 

Lakini wateja wenzake wamechoshwa kusubiri kwa muda mrefu. Baadhi yao wanajaribu kudanganya na muhudumu anarudisha nyuma mteja anayegandanya mbele ya pampu na kukwamisha shughuli.   

Caude Minani, mwendesha boda boda mwingine, anasema ametumia wiki nzima akiyatafuta lakini hajapata.   

Nilianzia jumapiki niko natafuta essence (mafuta)» mpaka saa hii. Nilipita Kamenge, nikapita Kinama, nikazunguka mpaka Ngagara, nikatoka Ngagara nikakamata basi ya kunifikisha hapa mjini. Nina muke na watoto watatu. Mi naona kwa hiyo tutakufa na njaa  

 

Hata hivyo waendesha bodaboda wengi sio wamiliki wa pikipiki wanazoendesha, kwani kila jioni wanapaswa kulipa kiasi fulani cha pesa kwa wamiliki.

Waendesha bodaboda kwenye mji wa Bujumbura, wakiwa wanasuburi kuwekewa mafuta kwenye mitungi yako.
Waendesha bodaboda kwenye mji wa Bujumbura, wakiwa wanasuburi kuwekewa mafuta kwenye mitungi yako. © FMM-RFI

Uhaba wa mafuta mbali na kukwamisha huduma za usafiri umezorotesha pia shughuli za kiuchumi nchini kote ambapo hivi  karibuni, Rais wa jamhuri Evariste Ndayishimiye, alitangaza kuwa uhaba uliopo ulisababishwa na Burundi kutokuwa na fedha za kigeni za kutosha.   

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.