Serikali ya Kenya yatakiwa kufanya juhudi za kudhibiti maambukizi zaidi ya UKIMWI
Dunia , Inapoadhimisha siku ya kimataifa kuhusu mapambano ya UKIMWI, mashirika ya kiraia yanayopambana na Ukimwi nchini Kenya yanahofu hatua zilizopigwa miaka 20, kudhibiti mambukizi mapya na vifo vinavyotokana na Ukimwi, huenda zikahujumiwa katika kipindi hiki cha janga la Corona.
Imechapishwa:
Tangu kuripotiwa kisa cha Kwanza cha virusi vya HIV nchini Kenya ,miaka 37 iliyopita, hatua muhimu zimepigwa kupambana na janga la UKIMWI na kudhibiti madhara yake.
Hata hivyo masharika ya kiraia nchini Kenya yanahisi hatua hizo chanya zinatishiwa na mvutano kati ya serikali na wafadhili
Patricia Asero ambaye ameishi na virusi vya HIV kwa zaidi ya miaka 20 anahofu kuwa hali iliyoshuhudiwa katika miaka ya nyuma, si kitu angependa kijurudie.
Na wanaharakati wanaopambana na Ugonjwa wa Kifua kikuu (TB) mojawapo ya magonjwa tegemezi miongoni mwa watu wanaoishi na virusi vya HIV nao wanaisihi serikali kutoipa nafasi TB kusababisha vifo zaidi .
Baraza linaloongoza mapambano dhidi ya UKIMWI Kenya, limerpoti maambukizi mapya zaidi ya elfu 41 mwaka wa 2021, huku kasi ya maambukizi ikiwa ni asilimia 4.9 . Idadi ya watu wanaoishi na virusi vya HIV nchini Kenya ni zaidi ya milioni moja nukta tatu