Pata taarifa kuu

Vita dhidi ya UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria vyapungua kwa sababu ya Covid-19

Janga la Covid-19 linaathiri vita dhidi ya magonjwa mengine. Hayo yamo katika ripoti ya kila mwaka ya Mfuko wa Kimataifa wa Kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria iliyotolewa Jumatano hii Septemba 8, 2021.

Mtoto huyu akipokea dozi ya chanjo ya malaria, Burkina Faso
Mtoto huyu akipokea dozi ya chanjo ya malaria, Burkina Faso AFP - OLYMPIA DE MAISMONT
Matangazo ya kibiashara

Matokeo yako wazi: Covid-19 imekuwa na "athari mbaya" kwenye mipango ya kuzuia magonjwa mengine ya mlipuko.

Jinsi ya kupambana na VVU / UKIMWI, malaria na kifua kikuu katikati ya janga la Covid-19? hali bado ni ngumu kukabiliana na magonjwa hayo ya mlipuko.

Mwaka jana, kwa mara ya kwanza katika miaka ishirini, viashiria vingi vya ufuatiliaji vilishuka. Takwimu za mwaka2020 "zinathibitisha kile kilichitia wasiwasi wakati Covid-19 ilipogundulika," amesema Peter Sands, mkurugenzi mtendaji wa Mfuko huo, aliyenukuliwa katika ripoti hiyo. “Athari za Covid-19 zimekuwa mbaya. Kwa mara ya kwanza katika historia yetu, viashiria vyetu vikuu vimeshuka ”.

"Athari kubwa"

Kwa mfano, mnamo mwaka 2020, idadi ya watu walio kuwa wakitibiwa kifua kikuu sugu kwa dawa ilipungua kwa 19%. Katika nchi ambazo Mfuko wa Kimataifa wa Kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria unawekeza, watu milioni 4.7 walio na ugonjwa huo wamepata matibabu, sawa na karibu milioni moja ikilinganishwa na mwaka 2019.

Huko Dakar, nchini Senegal, Serge Yotta, mkurugenzi wa muungano wa wanaharakati, Coalition Plus, amesema: "Vizuizi vya kusafiri vimekuwa na athari kubwa kwa sababu vituo vyetu vya afya vimekuwa na idadi watu wanaokuja kupatiwa huduma ya matibabu na halii hii imepunguza upatikanaji wa huduma za kimatibabu za msingi. "

Kinga dhidi ya Malaria imefanya kazi vizuri

Habari njema, hata hivyo, katika upungufu huu, kinga dhidi ya malaria imeendelea vizuri. “Wafanyakazi wa afya katika vijiji wamefaulu katika kurekebisha mipango ya kuzuia malaria. Kwa mfano nchini Benin, vyandarua vilisambazwa nyumba kwa nyumba baada ya marufuku ya watu kutembea kutokana na virusi vya Covid-19. Awali watu wengi walikuwa wakipuuzia wito wa kwenda kuchukuwa vyandarua katika vituo vya afya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.