Pata taarifa kuu
TANZANIA-HAKI

Naibu kiongozi wa chama cha CHADEMA Tundu Lissu afutiwa mashitaka dhidi yake

Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini imemfutia mashtaka naibu kiongozi wa chama cha upinzani cha CHADEMA nchini Tanzania, Tundu Lissu na wenzake watatu waliokuwa wakikabiliwa na mashtaka ya uchochezi. 

Tundu Lissu, ni wakili na mwanasiasa, lakini pia naibu kiongozi wa chama kikuu cha upinzani Tanzania cha CHADEMA.
Tundu Lissu, ni wakili na mwanasiasa, lakini pia naibu kiongozi wa chama kikuu cha upinzani Tanzania cha CHADEMA. Tundu Antiphas Lissu/twitter.com
Matangazo ya kibiashara

Hii ni baada ya Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania  kuanza kuchukua mwelekeo mpya kwa kesi zilizochukua muda mrefu mahakamani.

Mbali na kesi ya uchochezi dhidi ya Tundu Lissu na wenzake watatu, wahariri wa gazeti la Mawio, Jabiri Indrissa na Simon Mkina na mchapishaji wa kampuni ya Jamana Ismail Mehboo pia wamefutiwa mashitaka.

Tundu Lissu na wenzake watatu, walikuwa wanakabiliwa na mashtaka matano yanayohusiana na uchochezi wanayodaiwa kutenda mwaka 2016 kupitia gazeti la Mawio ambalo hata hivyo baadaye lilifutiwa usajili wake na serikali.

Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi hatua hiyo imekuja baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania (DPP) kuieleza mahakama kuwa hana nia ya kuendelea na mashtaka dhidi ya washtakiwa hao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.