Kiongozi wa chama cha CHADEMA Freeman Mbowe afikishwa mahakamani
Kiongozi wa upinzani nchini Tanzania, Freeman Mbowe, amefikishwa kwenye Mahakama Kuu kufunguliwa mashtaka ya ugaidi, ambayo chama chake cha upinzani CHADEMA kinasema yamechochewa kisiasa.
Imechapishwa:
Tangu Julai 21, Mbowe mwenye umri wa miaka 59 amekuwa akizuiwa baada ya kukamatwa jijini Mwanza akijiandaa kuwahotubia wanachama wa chama chake kushinikiza mabadiliko ya Katiba.
Wakati huo huo mawakili wa Freeman Mbowe wameiomba mahakama kumuachilia huru mteja wao wakidai mahakama hiyo haina mamalaka kisheria kusikiza kesi hiyo.
Peter kibatala anayeongoza jopo la mawakili wa Mbowe amewaambia waandishi habari kuwa endapo hoja zao zitakataliwa, wataendelea kuwapigania wateja wao kutumia vifungu vya sheria.
Shauri hilo lililosikilizwa kwa zaidi ya saa tatu limehudhuriwa na viongozi wengine wa vyama vya upinzani na wawakilishi wa baadhi ya balozi ikiwemo Uingereza na Marekani, asasi za kiraia na viongozi wa ngazi ya juu wa chama hicho.