Pata taarifa kuu
TANZANIA-HAKI

Tanzania : Ofisi ya mashitaka kutoa ushahidi katika kesi dhidi ya Freeman Mbowe

Nchini Tanzania, kiongozi wa mashtaka amesema mashahidi 24 na vielelezo 19, wanatarajia kutoa ushahidi katika kesi ya ugaidi na uhujumu uchumi inayomkabili, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Freeman Mbowe na wenzake watatu.

Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, Freeman Mbowe.
Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, Freeman Mbowe. RFI Kiswahli
Matangazo ya kibiashara

Upande wa utetezi unasema mashahidi wake ni pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Simon Sirro.

Hivi karibuni katika mkutano na waandishi wa habari, mkuu wa jeshi la polisi nchini Tanzania- IGP Simon Siro amesema kiongozi huyo wa upinzani sio malaika, na hivyo ni vyema kuiacha mahakama kutekeleza majukumu yake bila kuingiliwa.

Chama cha upinzani CHADEMA kinadai kesi dhidi ya kiongozi wake, imechochewa kisiasa.

Mashirika yanayotetea haki za binadamu yameikosoa vikali hatua ya Jeshi la Polisini nchini Tanzania ya kuwakamata baadha ya viongozi wa chama cha upinzani nchini humo Chadema.

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu nchini Tanzania na shirika kimataifa la Amnesty International ni miongoni mwa waliojitokeza na kupinga hatua hiyo.

Kwa upande wake, Amnesty International iliitaka serikali kusitisha mara moja kile ilichokiita kuendelea kudhibitiwa kwa upinzani nchini Tanzania.

Wito huu uliotolewa na mashirika haya, unakuja baada ya viongozi na wanachama kumi na mbili akiwemo kiongozi mkuu wa Chadema Freeman Mbowe kutiwa mbaroni huko jijini Mwanza usiku wa kuamkia tarehe 21 mwezi Julai.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.