Pata taarifa kuu
TANZANIA-USALAMA

Tanzania: Polisi yaonya wafuasi wa CHADEMA kuandamana Alhamisi

Jeshi la Polisi nchini Tanzania limesema halitakubali maandamano ya wafuasi wa chama kikuu cha upinzani CHADEMA, wakati kiongozi wao Freeman Mbowe atakapofikishwa tena Mahakama siku ya Alhamisi kwa madai ya ugaidi.

Freeman Mbowe, kiongozi wa chama kikuu cha upinzani CHADEMA, Dar es Salaam, Tanzania.
Freeman Mbowe, kiongozi wa chama kikuu cha upinzani CHADEMA, Dar es Salaam, Tanzania. Ericky Boniphace AFP/Archivos
Matangazo ya kibiashara

"Jeshi la polisi linatoa onyo kwa mtu au kikundi cha watu kitakachojaribu kuhamasisha mikusanyiko isiyo rasmi au kuandamana au namna yoyote ile kutoa shinikizo lolote," amesema Simon Sirro,Inspekta Jenerali wa Polisi nchini humo.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika alitangaza kuwa wafausi wa chama hicho washiriki kwenye maandamano ya amani kote nchini humo, kupinga mashtaka dhidi ya Mbowe ambayo chama chake kinasema ni ya uongo.

Madaktari nchini Nigeria wanaofanya kazi kwenye hopsitali za umma, wameanza mgomo usiogoma kudai nyongeza ya mshahara, bima ya afya na kulalamikia ukosefu wa vifaa kwenye vituo vya afya.

Rais wa chama  cha Madaktari nchini humo  Uyilawa Okhuaihesuyi ametangaza kuwa mgomo huo haujulikani utaisha lini.

Madaktari wamesisitiza kuwa, hawapo tayari kurejea kazini hata kwa wale wanaoshughulikia maambukizi ya Covid 19, wakati huu Madakatari wengine 19 wakipoteza maisha kutokana na virusi hivyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.