Pata taarifa kuu
TANZANIA-HAKI

Kesi ya Mbowe yaahirishwa hadi Ijumaa, wafuasi wake wakiona cha mtima kuni

Kesi kiongozi wa chama kikuu cha upinzani cha CHADEMA, Freeman Mbowe ambayo ilikuwa ikiendeshwa kwa njia ya mtandao imeahirishwa kutokana na changamoto za kimawasiliano. Mbowe anatarajiwa kufikishwa mahakamani siku ya Ijumaa asubuhi.

Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania CHADEMA Freeman Mbowe
Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania CHADEMA Freeman Mbowe Ericky Boniphace AFP/Archivos
Matangazo ya kibiashara

Freeman Mbowe anashtumiwa makosa ya ugaidi na uchumi. Kiongozi wa CHADEMA na wenzake kumi walikamatwa wiki mbili zilizopita huko Mwanza, mji wa kaskazini mashariki, ambapo walikuwa wakipanga mkutano wa kudai marekebisho ya katiba.

Hatua hiyo ya kumkamata Bw. Mbowe na wenzake kumi ililaaniwa na shirika la kimataifa la Haki za Binadamu la Amnesty International.

Tuhuma hizi zinaonekana kuwa ni za kisiasa, ameelezea Roland Ebole, mtafiti katika shirika hilo la haki za binadamu, akihojiwa na Christina Okello wa kitengo cha RFI katika kanda ya Afrika.

Wafuasi wa Mbowe ambao walikuwa wamekuja mahakamani kusikiliza ksi ya kiongozi wao wametawanywa na polisi, huku baadhi yao wakikamatwa, kulingana na vyanzo kadhaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.