Pata taarifa kuu
Uganda

Bobi Wine akamatwa na polisi Kampala

Mwanasiasa wa upinzani na aliyekuwa mgombea urais Robert Kyagulanyi, anayefahamika kwa jina maarufu Bobi Wine, amekamatwa jijini Kampala akiongoza maandamano kushinikiza kupatikana kwa wafuasi wake, waliotoweka.

Bobi Wine anainua mkono wakati wa kusikilizwa katika mahakama ya Kampala mnamo 29 Aprili 2019.
Bobi Wine anainua mkono wakati wa kusikilizwa katika mahakama ya Kampala mnamo 29 Aprili 2019. © AFP - Nicholas Bamulanzeki
Matangazo ya kibiashara

Watu kadhaa wamekamatwa wakiwemo wabunge zaidi ya kumi kutoka chama cha Bobi Wine cha National Unity Platformkulingana na duru kutoka kambi ya upinzani.

Vikosi vya usalama vilifyatua mabomu ya kutoa machozi na kutawanya waandamaji waliokuwa wameandamana na mwanasiasa huyo.

Bobi Wine anadai kuwa wafuasi wake walikamatwa na wakati wa kipindi cha kuelekea na baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika Januari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.