Pata taarifa kuu
UKRAINE-EU

Catherine Ashton kuelekea Ukraine kusaidia upatikanaji wa suluhu ya mgogoro uliosababisha maandamano makubwa

Mkuu wa sera za mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya EU, Catherine Ashton anatarajiwa kuwasili nchini Ukraine kesho jumanne kwa ziara ya siku mbili wakati maelfu ya waandamanaji wakiendelea kushinikiza Rais Viktor Yanukovych ajiuzulu baada ya kushindwa kutia saini makubaliano muhimu ya ushirikiano na Umoja wa Ulaya.

Matangazo ya kibiashara

Taarifa ya EU imesema Ashton akiwa nchini Ukraine anatarajiwa kukutana na pande zote zinazokinzana pamoja na wawakilishi wa asasi za kiraia.

Katika ziara hiyo Ashton atajaribu kusaidia upatikanaji wa suluhu ya mgogoro huo ambao umesababisha maandamano makubwa kwa takribani wiki mbili sasa.

Katika upande mwingine EU imesisitiza kuwa inataka kuendelezwa kwa uchunguzi wa ghasia zinazoendelea ili kubaini vitendo vya ukiukwaji wa binadamu vilivyofanyika.

Urusi kwa upande wake imekuwa ikiyataka mataifa ya Magharibi kutoingilia kati maandamaano yanayoendelea nchini Ukraine na badala yake taifa hilo liungane nao kufanya biashara.

Kutokana na hofu ya usalama, makumi ya wanajeshi wa Wizara ya ndani na polisi wa kutuliza ghasia wamepelekwa katika mji mkuu Kiev na wataendelea kusambazwa katika mitaa ya nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.