Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-KABUL

Rais Hamid Karzai ataka kuharakishwa kwa mchakato wa kuviondoa vikosi vya kigeni nchini humo kufuatia matukio ya hivi karibuni

Rais wa Afghanistan Hamid Karzai ametaka utekelezwaji wa kuviondoa vikosi vya majeshi ya kigeni nchini humo uongezwe kasi wakati huu ambapo kumezuka kashfa mpya dhidi ya wanajeshi wa Marekani walioko nchini humo. 

Rais wa Afghanistan Hamid Karzai
Rais wa Afghanistan Hamid Karzai Reuters/Omar Sobhani
Matangazo ya kibiashara

Kauli ya rais Karzai imekuja wakati ambapo gazeti moja la nchini Marekani likichapisha picha ambazo zinawaonesha wanajeshi wa Marekani wakiwamwagia mikojo wapiganaji wa kundi la Taliban baada ya kuwaua.

Kiongozi huyo amelaani vikali picha hizo na kusisitiza nji pekee ya kumaliza mateso ambayo wananchi wake wamekuwa wakiyashuhdia yakifanywa na majeshi ya kigeni nchini humo ni kuharakisha mpango wa kuviondoa vikosi hivyo nchini mwake.

Tayari serikali ya marekani kupitia kwa waziri wake mwa masuala ya ulinzi Leon Panetta imeomba radhi kwa matukio hayo na kuahidi kuwachukulia hatua wanajeshi waliousika.

Serikali ya Marekani na Afghanistan zimejikuta kwenye mzozo baada ya hapo awali mwanajeshi wake mmoja kutekeleza mauaji ya raia 16 wa Afghanistan hali iliyoilazimu serikali hiyo kuvitaka vikosi vya kigeni kufanya doria za mchana pekee.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.