Pata taarifa kuu

Australia: Mwanaume ashtakiwa kwa unyanyasaji wa kingono kwa watoto 91

Raia huyo wa Australia amepatikana na hatia ya makosa 1,623 yakiwemo ya ubakaji 136. Waathirika wake wachanga walikuwa wasichana wwenye umri wa mwaka mmoja.

Kati ya waathiriwa 91, 87 ni Waaustralia, na polisi inabaini kuwa wengine wanne walikuwa waathiriwa wa mtu huyo kati ya mwaka 2013 na 2014 alipofanya kazi ng'ambo kwa muda mfupi.
Kati ya waathiriwa 91, 87 ni Waaustralia, na polisi inabaini kuwa wengine wanne walikuwa waathiriwa wa mtu huyo kati ya mwaka 2013 na 2014 alipofanya kazi ng'ambo kwa muda mfupi. REUTERS - LOREN ELLIOTT
Matangazo ya kibiashara

Mfanyikazi wa zamani wa kulea watoto nchini Australia ameshtakiwa kwa unyanyasaji wa kingono kwa watoto 91, katika kile polisi walichoelezea Jumanne kama moja ya kesi "ya kutisha zaidi" ya unyanyasaji wa watoto ambayo hayajawahi kutokea nchini. Uhalifu huo ulifanyika katika vituo kumi tofauti vya kulelea watoto kati ya mwaka 2007 na 2022 na yalilenga pekee "wasichana waliozaliwa, kulingana na polisi. Waathiriwa wachanga zaidi walikuwa na umri wa mwaka mmoja.

Mtu huyo mwenye umri wa miaka 45 ameshtakiwa kwa makosa 1,623 ya uhalifu yakiwemo ubakaji 136 na vitendo 110 vya ngono na watoto walio chini ya umri wa miaka kumi, polisi imeongeza.

Maelfu ya picha zilipatikana kwenye kompyuta na simu yake

Wachunguzi wamemkamata baada ya kupata ponografia ya watoto kwenye eneo la Darkweb ambaye historia yake ilisaidia kufuatilia njia hadi kwenye eneo la Brisbane, jiji lenye watu wengi zaidi katika jimbo la magharibi la Queensland. Zaidi ya picha na video 4,000 ziligunduliwa kwenye simu na kompyuta yake, huku maafisa wakipima uzito wa madai ya uhalifu "wa kuchukiza" aliyoufanya mfanyakazi huyo wa zamani wa kulea watoto.

Kati ya waathiriwa 91, 87 ni Waaustralia, na polisi inaamini kuwa wengine wanne walikuwa waathiriwa wa mtu huyo kati ya mwaka 2013 na 2014 alipofanya kazi ng'ambo kwa muda mfupi. Polisi imesema imekuwa ikishirikiana na mashirika ya kimataifa kutafuta waathiriwa hao wanne, lakini hawakufichua ni nchi zipi zinazozingatiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.