Pata taarifa kuu
DIPLOMASIA-ULINZI

Australia yapinga ujenzi wa ubalozi mpya wa Urusi

Serikali ya Australia imeeleza chaguo lake kwa kuzua tishio kwa usalama wa taifa lake, katika muktadha wa vita vya Ukraine. Mvutano wa kidiplomasia unahusishwa na vita vya Ukraine. Serikali ya Australia itapinga ujenzi wa ubalozi mpya wa Urusi karibu na Bunge huko Canberra, Waziri Mkuu Anthony Albanese ametangaza leo Alhamisi, Juni 15, akitaja hatari ya usalama wa kitaifa.

Waziri Mkuu wa Australia Anthony Albanese ametangaza kwamba baada ya kuchunguza njia zote za kisheria bila mafanikio, sheria mpya zitapitishwa na Bunge kuzuia ujenzi wa ubalozi wa Urusi kwenye ardhi hii.
Waziri Mkuu wa Australia Anthony Albanese ametangaza kwamba baada ya kuchunguza njia zote za kisheria bila mafanikio, sheria mpya zitapitishwa na Bunge kuzuia ujenzi wa ubalozi wa Urusi kwenye ardhi hii. AP - Vincent Thian
Matangazo ya kibiashara

"Serikali imepokea ushauri wa wazi wa usalama kuhusu hatari inayoletwa na uwepo mpya wa Urusi karibu na bunge," Anthony Albanese amewaambia waandishi wa habari. Kwa sasa Urusi inakodisha nyumba karibu na Bunge huko Canberra. Serikali ya Australia tayari imejaribu, bila mafanikio, kufuta ukodishaji huu, uliotiwa saini kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 2008.

Mkuu wa serikali ya Australia ametangaza kwamba baada ya kuchunguza njia zote za kisheria bila mafanikio, sheria mpya zitapitishwa na Bunge kuzuia ujenzi wa ubalozi wa Urusi kwenye ardhi hii. "Tunachukua hatua haraka ili kuhakikisha kuwa eneo lililokodishwa haliwi uwepo rasmi wa kidiplomasia," waziri mkuu amesema.

Tishio kwa usalama wa taifa

Kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Ndani wa Australia, Clare O'Neil, ubalozi mpya ambao Urusi inataka kujenga ni tishio la wazi kwa usalama wa kitaifa wa nchi.

"Tatizo kuu la mrad wa ujenzi wa ubalozi wa pili wa Urusi huko Canberra ni eneo kutakojengwa ubalozi huo," amesema. "Eneo hilo liko karibu moja kwa moja na makao makuu ya Bunge," Clare O'Neil amebaini. Ubalozi wa sasa wa Urusi uko katika wilaya ya Griffith kusini mwa jiji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.