Pata taarifa kuu

Marekani kusaidia Australia kuongeza utengenezaji wa makombora

Washington itaimarisha hifadhi yake ya silaha kwa kuisaidia Australia kujenga viwanda vya kutengeneza makombora, maafisa wamesema baada ya mazungumzo ya ngazi ya juu kati ya nchi hizo mbili siku ya Jumamosi. "Tunatarajia utengenezaji wa makombora kuanza nchini Australia ndani ya miaka miwili, kama sehemu ya msingi wa viwanda kati ya nchi zetu mbili," Waziri wa Ulinzi wa Australia Richard Marles amewaambia waandishi wa habari.

Waziri wa Ulinzi wa Australia Richard Marles anashiriki mkutano wa pamoja wa waandishi wa habari na mawaziri wa Mambo ya Nje na Ulinzi wa Ufaransa Quai d'Orsay huko Paris, Ufaransa, Januari 30, 2023.
Waziri wa Ulinzi wa Australia Richard Marles anashiriki mkutano wa pamoja wa waandishi wa habari na mawaziri wa Mambo ya Nje na Ulinzi wa Ufaransa Quai d'Orsay huko Paris, Ufaransa, Januari 30, 2023. REUTERS - SARAH MEYSSONNIER
Matangazo ya kibiashara

Uzalishaji unatarajiwa kuanza "ndani ya miaka miwili," Waziri wa Ulinzi wa Australia Richard Marles aliwaambia waandishi wa habari Jumamosi, kama sehemu ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili. Australia itatengeneza mifumo mingi ya roketi.

"Tumefurahishwa sana na hatua tunazochukua kuelekea kuanzisha biashara ya kuongozwa na silaha za milipuko katika nchi hii," ameongeza. Australia itatengeneza Mifumo ya Roketi ya sehemu nyini za kurushia (GMLRS).

Kama sehemu ya tangazo hilo, lililofuatia majadiliano na Bw. Marles na Waziri wa Mambo ya Nje wa Australia Penny Wong, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken na Mkuu wa Pentagon Lloyd Austin wamezuru Brisbane siku ya Jumamosi.

Viwanda changa

Ushirikiano huu utaiwezesha Australia kukuza tasnia yake mpya ya makombora ya ndani na kuhakikisha usambazaji wa kuaminika kwa vikosi vya jeshi la Marekani katika siku zijazo.

Hatua hii inakuja katikati ya hali ya vita nchini Ukraine, ambayo imedhoofisha ugavi wa kijeshi nchini Marekani, na kupunguza hatua kwa hatua hifadhi yake ya makombora na risasi nyingine.

Australia kwa sasa inaboresha vikosi vyake vyenye silaha, ikielekea kwenye uwezo wa jaribuo la urushaji makombora ya masafa marefu ili kuwaepusha maadui watarajiwa kama vile China.

Canberra pia imekubali kukarabati kambi muhimu za kijeshi kaskazini mwa nchi hiyo ili ziweze kuandaa mazoezi ya mafunzo na kuruhusu kuongezeka kwa mzunguko wa wanajeshi wa Marekani. "Tumepata maendeleo makubwa katika mipango ya mkao wa nguvu ya Marekani," Bw. Marles alisema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.