Pata taarifa kuu

Macron na Biden wakutana Roma kwa lengo la kukomesha uhasama

Emmanuel Macron na Joe Biden wamekutana mjini Roma Ijumaa hii, Oktoba 29, 2021. Ziara hii kati ya wakuu wa nchi za Ufaransa na Marekani, iliyoandaliwa kwa minajili ya kutafutia ufumbuzi uhasama baina ya nchi hizi mbili baada ya mzozo wa nyambizi za Australia, ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu upande wa Ufaransa.

Joe Biden na Emmanuel Macron, Oktoba 29, 2021 huko Roma.
Joe Biden na Emmanuel Macron, Oktoba 29, 2021 huko Roma. AFP - LUDOVIC MARIN
Matangazo ya kibiashara

Picha hii ya Emmanuel Macron na Joe Biden wakipeana mikono, inaashiria kulingana na mtazamo wa Ufaransa kwamba rais wa Marekani anataka kufanya juhudi baada ya hasira kubwa ya Paris, katikati ya mwezi Septemba, kufuatia tangazo la uvunjaji wa kile kilichoelezwa kuwa "mkataba wa karne". Australia, ambayo ilikuwa inunue nyambizi za Ufaransa, ilivunja mkataba bila kuitaarifu  Paris na kutia saina kwenye mkataba na Marekani.

Baada ya kisa hiki Ufaransa iliwarejesha nyumbani mabalozi wake nchini Marekani na Australia kwa kuonyesha ghadhabu zake, ishara kubwa ya kidiplomasia dhidi ya mshirika kama Marekani. Joe Biden alielewa mara moja ujumbe huo na akaomba kuzungumza na Emmanuel Macron kwenye simu kuweza kujieleza. Rais wa Ufaransa alimfanya asubiri kwa siku kadhaa kabla ya kuzungumza naye.

Simu hii ilikuwa hatua ya kwanza kuelekea maridhiano. Hapo ndipo ilipoamuliwa kupanga mkutano kati ya marais hao wawili. Na mkutano huu, hatimaye umefanyika huko Roma kando ya mkutano wa G20 Ijumaa hii. Lakini alichotaka Emmanuel Macron ilikuwa mkutano huo ufanyike katika eneo la Ufaransa, mjini Roma.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.