Pata taarifa kuu

Australia, Marekani na Uingereza zaungana kuhusu mradi wa nyuklia wa manowari

Ushirikiano 'usio na kifani' kati ya Marekani, Uingereza na Australia umetangazwa huko California, nchini Marekani: Rais wa Marekani Joe Biden alizindua mpango wa kuvutia wa manowari unaotumia nguvu za nyuklia Jumatatu Machi 13 kwa ushirikiano na Australia na Uingereza, iliyokusudiwa kukabiliana na China katika kanda ya bahari ya India na ile ya Pacific.

Nyambizi tano za kisasa ziitwazo Virginia (kwenye picha) zitatengenezwa kwa ajili ya Australia kabla ya nchi hii na Uingereza na Marekani kufanya kazi pamoja kubuni kizazi kipya cha manowari.
Nyambizi tano za kisasa ziitwazo Virginia (kwenye picha) zitatengenezwa kwa ajili ya Australia kabla ya nchi hii na Uingereza na Marekani kufanya kazi pamoja kubuni kizazi kipya cha manowari. AP - Amanda Gray
Matangazo ya kibiashara

"Tunajiweka katika nafasi nzuri zaidi ya kukabiliana pamoja na changamoto za leo na kesho," rais wa Marekani amesema kutoka kituo cha jeshi la wanamaji huko San Diego, Marekani akiambatana na Rishi Sunak na Waziri Mkuu wa Australia Anthony Albanese.

Joe Biden amehakikisha kwamba Marekani inapaswa kuwa na "marafiki bora", akisifu muungano huu wa pande tatu uitwao Aukus, ambao ulikuwa umeikasirisha Ufaransa ulipotangazwa miezi kumi na minane iliyopita.

Akizungumza na viongozi wengine mjini San Diego, California, Rais wa Marekani Joe Biden alisisitza kwamba maboti hayatakuwa na silaha za nyuklia na hayatabadilisha sera ya Austaralia ya kuwa nchi isiyokuwa na nyuklia.

Waziri Mkuu wa Australia alisisitiza kuwa nchi yake ilikuwa inafanya "uwekezaji mkubwa zaidi katika historia [yake]" kupitia Aukus, ambayoilijikuta ikinunua manowari za Kimarekani zinazotumia nguvu za nyuklia kabla ya kutengeneza yenyewe meli za kizazi kipya.

Mwenzake wa Uingereza pia amesifu juhudi zinazofanywa na Uingereza kuongeza bajeti yake ya ulinzi, na kubaini kuwa pamoja na Marekani na Australia, nchi yake imejitolea kwa "makubaliano ya ulinzi wa pande nyingi muhimu zaidi kwa vizazi kadhaa.

Katika kipindi cha miezi 18 iliyopita, changamoto tunazokabiliana nazo zimeongezeka.

Chini ya mkataba ulioainishwa Jumatatu , wanajeshi wa majini wa kikosi cha Australia - Royal Australian Navy (RAN) watafanya kazi na vikosi vya Marekani na Uingereza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.