Pata taarifa kuu

Mifumo ya ulinzi wa anga ya Ukraine yadungua kombora za Urusi

Mifumo ya ulinzi wa anga ya Ukraine imedungua "kombora kadhaa za Urusi" juu ya anga ya mji wa Kyiv, meya wa mji mkuu wa Ukraine, Vitaly Klitschko, amesema. Milipuko kadhaa ilisikika mapema alasiri katika mji mkuu wa Ukraine na waandishi wa habari wa AFP.

Maafisa wa idara ya Zima moto wakifanya kazi baada ya shambulio la ndege isiyo na rubani kwenye majengo huko Kyiv, Ukraine, Oktoba 17, 2022.
Maafisa wa idara ya Zima moto wakifanya kazi baada ya shambulio la ndege isiyo na rubani kwenye majengo huko Kyiv, Ukraine, Oktoba 17, 2022. AP - Roman Hrytsyna
Matangazo ya kibiashara

Kamanda wa vikosi vya Urusi nchini Ukraine anasema hali katika mji wa kusini wa Kherson ni "ngumu" na wakaazi wanapaswa kuhamishwa.

Akizungumza kwenye TV ya serikali ya Urusi, Jenerali Sergei Surovikin alisema wanajeshi wa Ukraine wanaotumia roketi za Himars walikuwa wakigonga miundombinu na makazi ya jiji hilo.

"Jeshi la Urusi juu ya yote litahakikisha uokoaji salama wa watu" wa Kherson, alisema.

Wakati huo huo Rais wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen ameyaita mashambulizi ya Urusi yanayolenga miundombinu ya umma nchini Ukraine kuwa ni uhalifu wa kivita. Von der Leyen amesema mapema leo akiwa mjini Strasbourg kwamba wameshuhudia Urusi ikifanya mashambulizi ya kulenga miundombinu ya umma na hatua hiyo inaashiria ukurasa mpya katika kile alichokielezea kama vita vya kikatili. Aidha kiongozi huyo amerudia matamshi yake kwamba Umoja wa Ulaya utaendelea kuiunga mkono Ukraine kadiri itakavyowezekana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.