Pata taarifa kuu

Diplomasia ya Ukraine yampendekezea Volodymyr Zelensky kuvunja uhusiano na Tehran

Kyiv inaishtumu Iran kwa kuipa Urusi ndege zisizokuwa na rubani (drone) kuishambulia Ukraine katika wiki za karibuni.  Wakati huo huo Rais Zelensky amesema adui anaweza kuyashambulia miji nchini humo lakini kamwe hatofanikiwa kuwagawa Waukraine.

Rais Volodymyr Zelensky katika picha iliyotolewa na idara inayohusika na masuala ya vyombo vya habari katika ofisi ya rais wa Ukraine mnamo Julai 23, 2022.
Rais Volodymyr Zelensky katika picha iliyotolewa na idara inayohusika na masuala ya vyombo vya habari katika ofisi ya rais wa Ukraine mnamo Julai 23, 2022. AFP - STR
Matangazo ya kibiashara

Ukraine imeendelea kukumbwa na mashambulizi mabaya. Mashambulizi hayo yameshuhudiwa katika miji mbalimbali ya nchi hiyo

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameyalaani mashambulizi hayo na kuyaita ya kigaidi dhidi ya raia wa taifa lake. Katika mtandao wake wa Telegram, rais Zelensky amesema adui anaweza kuyashambulia miji nchini humo lakini kamwe hatofanikiwa kuwagawa Waukraine.

Siku ya Jumatatu, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alisema droni za Iran zilitumika katika mashambulizi yaliyofanywa na Russia katika miundo mbinu ya miji kadhaa ya Ukraine.

Mwezi uliopita, Kyiv iliamua kuchukua hatua muhimu kupunguza uhusiano wa kidiplomasia na Tehran kufuatia madai ya nchi hiyo kupelekea silaha mbalimbali Russia.

Iran ilisema uamuzi huo ulikuwa “unamsukumo wa taarifa zisizokuwa na msingi zilizoenezwa na propaganda za vyombo vya habari vya kigeni.”

Mwezi Septemba, Marekani iliiwekea vikwazo kampuni iliyokuwa ikiituhumu inasaidia kusafirisha droni za Iran kwenda Russia ili zitumike nchini Ukraine.

Wanajeshi wa Urusi walishambulia maeneo ya Kyiv na Odesa nchini Ukraine kwa makombora wakitumia ndege zisizokuwa na rubani za Iran.

Maafisa wa Ukraine walisema kwamba utawala wa Moscow umeendelea kuangusha makombora nchini Ukraine na kusababisha vifo na uharibifu mkubwa kwa siku ya nne mfululizo.

Moscow ilisema inaangusha makombora hayo nchini Ukraine kufuatia kuharibiwa kwa daraja linalounganisha Urusi na Crimea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.