Pata taarifa kuu

Ukraine: Jeshi la Urusi lakiri kuanza kuhamisha wakazi wa Kherson

Rais wa Urusi Vladimir Putin ameagiza kuanzishwa kwa sheria ya kijeshi katika maeneo manne yaliyounganishwa. Utawala wa uvamizi wa Urusi huko Kherson, kusini mwa Ukraine, umesema Jumatano kwamba ulikuwa ukiuhamisha wakazi wa mji huo unaokabiliwa na mashambulizi ya wanajeshi wa Ukraine ambao wanaosonga mbele, huku wakihakikisha kwamba jeshi la Urusi litapigana katika mji huo "hadi kifo". Kwa upande wake, Kyiv imeshutumu Urusi kwa "kujaribu kuwatisha" wakazi wa mji wa Kherson.

Utawala wa uvamizi wa Urusi huko Kherson, kusini mwa Ukraine, umesema Jumatano (tarehe 19 Oktoba) kwamba ulikuwa ukihamisha wakazi wa mji unaokabiliwa na mashambulizi ya wanajeshi wa Ukraine wanaosonga mbele.
Utawala wa uvamizi wa Urusi huko Kherson, kusini mwa Ukraine, umesema Jumatano (tarehe 19 Oktoba) kwamba ulikuwa ukihamisha wakazi wa mji unaokabiliwa na mashambulizi ya wanajeshi wa Ukraine wanaosonga mbele. REUTERS - ALEXANDER ERMOCHENKO
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Urusi Vladimir Putin ameamuru Jumatano hii, Oktoba 19 kuanzishwa kwa sheria ya kijeshi katika maeneo manne ya Ukraine ya Donetsk, Lugansk, Kherson na Zaporizhia yaliyotwaliwa na Moscow mwezi Septemba.

Vladimir Putin ametangaza hatua hii wakati wa kikao chake cha Baraza lake la Usalama lililotangazwa kwenye televisheni. Kremlin saa chache baadae ilitangaza kuanza kutumika kwa sheria ya kijeshi katika maeneo haya kuanzia Alhamisi usiku wa manane.

"Ningependa kukukumbusha kwamba katika Jamhuri ya Watu wa Donetsk, Jamhuri ya Watu wa Luhansk, na pia katika mikoa ya Kherson na Zaporizhia, utawala wa sheria za kijeshi ulikuwa tayari unatumika kabla ya kuunganishwa kwa majimbo hayo na Urusi. Tunachofanya sasa ni kurasimisha utawala huu chini ya sheria ya Urusi."

Maeneo haya "yalianzisha sheria ya kijeshi kabla ya kushikamana na Shirikisho la Urusi, lakini ni muhimu kurasimisha utawala huu kwa kufuata sheria za Kirusi", amesema Vladimir Putin. Amehalalisha hatua hii kwa kusema kwamba Kyiv ilikataa kufanya mazungumzo na Moscow na iliendelea kulingana na rais wa Urusi "kushambulia" raia katika majimbo haya. "Ukraine inaojifananisha na utawala wa kinazi inatumia kwa uwazi mbinu za kigaidi (...) inatuma makundi ya wahujumu katika eneo letu," ameongeza, akilaani hasa shambulio dhidi ya daraja la Crimea na "miundombinu ya nyuklia", bila kutaja ipi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.