Pata taarifa kuu

Ukraine: Jeshi la Urusi latangaza "uhamisho salama wa wakazi wa" Kherson

Jeshi la Urusi linajiandaa kuwahamisha wakazi wa mji wa Kherson, mji mkuu wa jimbo la jina moja lililotwaliwa na Urusi kusini mwa Ukraine, kutokana na mashambulizi kutoka Kyiv, ametangaza Jumanne kamanda wa vikosi vya Urusi nchini Ukraine.

Wanajeshi wa Urusi wakilinda eneo wakati kundi la waandishi wa habari wa kigeni wakitembelea Kherson, eneo la Kherson, kusini mwa Ukrainia, Mei 20, 2022.
Wanajeshi wa Urusi wakilinda eneo wakati kundi la waandishi wa habari wa kigeni wakitembelea Kherson, eneo la Kherson, kusini mwa Ukrainia, Mei 20, 2022. AP
Matangazo ya kibiashara

"Jeshi la Urusi litahakikisha juu ya uokoaji wote salama wa raia" kutoka mji huu ambapo mashambulizi ya Ukraine dhidi ya miundombinu ya raia husababisha, kulingana na Jenerali Sergei Surovikin, "tishio la moja kwa moja kwa maisha ya wakaazi". Hiki ndicho alichoambia kituo cha televisheni cha umma cha Urusi Rossia 24, akisisitiza kuwa hali ya mji ni "tete".

"Hali katika eneo la operesheni maalum ya kijeshi inaweza kuelezwa kuwa ya wasiwasi. Adui haachi majaribio yake ya kushambulia maeneo ya wanajeshi wa Urusi,” amesema Bw. Surovikin, ambaye amekuwa akisimamia operesheni za vikosi vya Urusi nchini Ukraine kwa siku kumi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.