Pata taarifa kuu

China yapunguza ushirikiano na Marekani baada ya ziara ya Pelosi Taiwan

Matokeo ya ziara ya Nancy Pelosi mapema wiki hii nchini Taiwan, kisiwa kinachochukuliwa na China kuwa mkoa wa waasi, yanaendelea kuhisiwa. Baada ya kuamua kumuwekea vikwazo spika wa Baraza la Wawakilishi, Beijing imetangaza kusitisha ushirikiano wote na Marekani kuhusu suala la ongezeko la joto na sekta nyingine, na hivyo kusababisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili unaporomoka hadi kiwango cha chini kabisa.

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi akihudhuria mkutano na waandishi wa habari pembezoni mwa mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa Asia Mashariki huko Phnom Penh tarehe 5 Agosti 2022.
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi akihudhuria mkutano na waandishi wa habari pembezoni mwa mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa Asia Mashariki huko Phnom Penh tarehe 5 Agosti 2022. AFP - TANG CHHIN SOTHY
Matangazo ya kibiashara

Hatua mpya imefikiwa katika kuzorota kwa biashara kati ya mataifa hayo mawili makubwa.

Beijing imeamua kusitisha ushirikiano na Washington katika katika skta kadhaa, ikiwa ni pamoja na sekta ya mapambano dhidi ya ongezeko la joto duniani, huku nchi hizo mbili zikiwa ni wachafuzi wa kwanza duniani.

Lakini juu ya yote, China itafuta mazungumzo kati ya viongozi wa kijeshi na mikutano miwili ya nchi mbili kuhusu usalama.

Haya yote katika hali ambayo mvutano umeongezeka baada ya ziara ya Nancy Pelosi hukoTaiwan, ambayo Beijing inachukuliwa kuwa sehemu muhimu ya ardhi yake. Ziara ya Bii Pelosi huko Taiwan ilionekana kama uchochezi kwa upande wa serikali ya kikomunisti, ambayo inalaani shambulio dhidi ya uhuru wake.

Kwa upande wake, Washington haijaijikurubisha na imemuita balozi wa China Qin Gang kupinga dhidi ya mazoezi ya kijeshi ya China. "Tumeshutumu operesheni za kijeshi za China, ambazo ni za kutowajibika na kinyume na lengo letu la muda mrefu la kudumisha amani na utulivu katika Mlango wa Bahari wa Taiwan," msemaji wa serikali anayesimamia Masuala ya usalama wa kitaifa, John Kirby.

Jeshi la China limeanzisha operesheni za majini na angani kwenye pwani ya Taiwan kwa lengo la kulipiza kisasi ziara ya spika wa Bunge la Marekani Nancy Pelosi. Makombora ya China, kwa mara ya kwanza, yamerushwa juu ya anga ya kisiwa hicho, kulingana na propaganda za kikomunisti ambazo zinaripoti operesheni za kiwango ambacho hakijawahi kutokea katika eneo hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.