Pata taarifa kuu

Jeshi la Taiwan: Tunajiandaa kwa vita bila kukusudia

Vikosi vya jeshi vya Taiwan vimesema leo Alhamisi "kujiandaa kwa vita bila kukusudia" wakati China ikianza mazoezi makubwa zaidi ya kijeshi katika historia ya nchi hiyo kwa kuzingira kisiwa hicho. 

Watalii wanatazama helikopta ya kijeshi ya China ikipita kwenye Kisiwa cha Pingtan, mojawapo ya maeneo ya karibu zaidi ya China na Taiwan, katika mkoa wa Fujian, Agosti 4, 2022.
Watalii wanatazama helikopta ya kijeshi ya China ikipita kwenye Kisiwa cha Pingtan, mojawapo ya maeneo ya karibu zaidi ya China na Taiwan, katika mkoa wa Fujian, Agosti 4, 2022. AFP - HECTOR RETAMAL
Matangazo ya kibiashara

"Wizara ya Ulinzi wa Kitaifa inasisitiza kwamba itazingatia kanuni ya kujiandaa kwa vita bila kukusudia," Wizara ya Ulinzi ya Taiwan imesema katika taarifa.

Wakati huo huo China ''imetuma ndege 27 za kivita katika anga ya Taiwan'' baada ya Pelosi kuondoka, kulingana na taarifa iliyotolewa na Taiwan.

Wizara ya Ulinzi ya Taiwan ilisema ujumbe wa hivi punde zaidi wa China ni pamoja na ndege 16 za kivita aina ya Sukhoi-30 na aina nyingine 11.

Beijing imeelezea hasira yake juu ya ziara ya Spika wa Bunge Nancy Pelosi nchini Taiwan, ziara ya afisa wa  ngazi ya juu wa Marekani katika kisiwa hicho kwa miaka 25, kwa kutangaza mfululizo wa mazoezi ya kijeshi ambayo itafanya karibu na Taiwan.

Beijing inaichukulia Taiwan kama eneo la Uchina, lakini Taiwan inakataa madai ya China na kuapa kujitetea.

Pelosi alisema mwishoni mwa ziara yake nchini Taiwan kwamba China haiwezi kuzuia viongozi wa dunia kuzuru kisiwa hicho.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.