Pata taarifa kuu

China yaendelea kuonywa kuhusu mazoezi yake ya jeshi karibu na Taiwan

Taiwan inasema ndege za kivita na manuari za kivita za China, zimevuka mpaka na kuingia katika eneo lake, hatua inayosema ni chokochoko. 

Helikopta za kijeshi za China zinapaa juu ya Kisiwa cha Pingtan karibu na Taiwan katika Mkoa wa Fujian mnamo Agosti 4, 2022.
Helikopta za kijeshi za China zinapaa juu ya Kisiwa cha Pingtan karibu na Taiwan katika Mkoa wa Fujian mnamo Agosti 4, 2022. AFP - HECTOR RETAMAL
Matangazo ya kibiashara

Hili limethibitishwa na Wizara ya Ulinzi ya Taiwan siku ya Ijumaa, wakati huu China ikisema itaendelea na mazoezi hayo licha ya  kulaaniwa na Marekani, Japan na Umoja wa Ulaya. 

Uamuzi wa Beijing unakuja  baada ya ziara ya spika wa bunge la Marekani Nancy Pelosi, katika kisiwa hicho na kupata fursa ya kuwahotubia wabunge. 

Marekani inasema baada ya ziara ya Pelosi, China haikupaswa kuchukua hatua hii inayosema haikubaliki. 

Japan kwa upande wake  inasema hatua ya Beijing ni tishio la kiusalama katika ukanda huo na kutaka lisitishwe. 

Hata hivyo jeshi la China linasema litaendelea na mazoezi haya mpaka siku ya Jumapili, ikiendelea kusisitiza kuwa Taiwan ni sehemu ya nchi yake. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.