Pata taarifa kuu
USALAMA-DIPLOMASIA

Taiwan: China yarusha makombora mengi ya balestiki katika mazoezi makubwa

Jeshi la China limeanza Alhamisi, Agosti 4, mazoezi muhimu zaidi ya kijeshi katika historia yake karibu na Taiwan, jibu la nguvu kwa ziara ya Spika wa Bunge la Wawakili la Marekani, Nancy Pelosi, kisiwani humo. 

Helikopta za kijeshi za China zaruka juu ya Kisiwa cha Pingtan, mojawapo ya maeneo ya karibu zaidi ya China na Taiwan, katika jimbo la Fujian mnamo Agosti 4, 2022, kabla ya mazoezi makubwa ya kijeshi kwenye pwani ya Taiwan.
Helikopta za kijeshi za China zaruka juu ya Kisiwa cha Pingtan, mojawapo ya maeneo ya karibu zaidi ya China na Taiwan, katika jimbo la Fujian mnamo Agosti 4, 2022, kabla ya mazoezi makubwa ya kijeshi kwenye pwani ya Taiwan. AFP - HECTOR RETAMAL
Matangazo ya kibiashara

Vikosi vya jeshi la China vimerusha makombora "mengi" ya Balestiki katika maji yanayozunguka Taiwan wakati wa mazoezi yao makubwa, Wizara ya Ulinzi ya Taipei imesema, ikilaani "vitendo visivyo vya busara vinavyodhoofisha amani ya kikanda".

Ikiwa safari yake katika eneo hili linalodaiwa na China kuwa ni moja ya maeneo yake ilidumu chini ya saa ishirini na nne, Bi Pelosi alizua ghadhabu ya Beijing kwa kuwa afisa wa juu zaidi wa Marekani aliyechaguliwa kuzuru Taipei katika miaka 25. Alisisitiza kwamba Marekani haitakiacha kisiwa hicho, kinachotawaliwa na serikali ya kidemokrasia na ambayo inaishi chini ya tishio la mara kwa mara la uvamizi wa jeshi la China.

Kwa kujibu, Beijing imezindua kuanzia Alhamisi mapema asubuhi mazoezi makubwa ya kijeshi katika maeneo sita karibu na Taiwan, kwenye barabara za biashara zenye shughuli nyingi. "Mazoezi yanaanza" na yataendelea hadi Jumapili mchana, televisheni ya taifa ya China CCTV imesema katika ujumbe kwenye mitandao ya kijamii. "Katika kipindi hiki, meli na ndege husika hazipaswi kuingia kwenye maji na anga kunakofanyika mazoezi hayo. "

"Wizara ya Ulinzi wa Kitaifa imesema kwamba Chama cha Kikomunisti cha China kimerusha makombora mengi ya balestiki ya Dongfeng katika maji yanayozunguka kaskazini-mashariki na kusini-magharibi mwa Taiwan kuanzia saa 1:56 mchana saa za China (sawa na saa 5:56 asubuhi saa za kimataifa)," Wizara ya Ulinzi ya Taipei imesema katika taarifa fupi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.