Pata taarifa kuu

China yaanza luteka ya kijeshi kufuatia ziara ya Nancy Pelosi Taiwan

China imepanga kuanza mazoezi ya kijeshi baharini,  karibu na Taiwan baada ya ziara ya spika wa bunge la Marekani, Nancy Pelosi.  

Guaride la jeshi la China.
Guaride la jeshi la China. REUTERS/ David Gray
Matangazo ya kibiashara

Mazoezi haya yatakayoanza leo mchana  kwa mujibu wa Beijing , ni pamoja na  kurusha makombora ya masafa marefu ambayo hayajawahi kushuhudiwa katika miaka ya hivi karibuni. 

Rais wa Taiwan Tsai Ing Wen amethibitisha hatua hiyo ya China, akisema nchi yake tangu ziara hiyo ya spika Pelosi, imeendelea kupata vitisho vya kijeshi.  

Taipei imesema ilibidi kufanya doria za ndege za kivita ,siku ya Jumatano kujaribu kukabili ndege za kivita za China. 

Aidha, zisizo na rubani zimekuwa zikionekana katika kisiwa cha Kinmen karibu na Taiwan na hii ikijiri baada ya uvamizi wa mtandao kwenye mitandao ya kiserikali.  

Mshauri wa maswala ya usalama nchini Marekani ,Jake Sullivan ,ameonya  mazoezi hayo yanaweza kuvuka mipaka, huku  Joseph Borrell Mkuu wa sera ya nje ya Umoja wa Ulaya akisema, China haina sababu ya kuandaa mazoezi. 

Msemaji wa serikali ya Côte d'Ivoire, Amadou Coulibaly amethibitisha hilo na kusema juhudi zinafanyika ili kuwaachia wanajeshi hao ili waungane tena na familia zao. 

Wanajeshi hao walikamatwa jijini Bamako tarehe 10 mwezi Julai, na kudaiwa ni mamluki waliokuwa na njama ya kuiangusha serikali ya kijeshi. 

Hata hivyo, wanajeshi hao walidai walikuwa katika kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa MINUSMA, na uwepo wao ulilenga kusaidia kupambana na makundi ya kijihadi. 

Ripoti zinasema jitihada za nchi ya Togo chini ya rais Faure Gnassingbé, kujaribu kusuluhisha mvutano huu kati ya Mali na Côte d'Ivoire hazijazaa matunda mpaka sasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.