Pata taarifa kuu

China yaizingira Taiwan kwa mazoezi ya kijeshi

Ziara ya Nancy Pelosi, Spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani katika Kisiwa cha Taiwan, imelaaniwa na China, ambayo imeamuru hasa mazoezi ya kijeshi ya baharini na anga karibu na Taiwan pamoja na majaribio ya kawaida ya makombora katika bahari ya mashariki mwa Taiwan.

Wahudumu wa chombo cha kurusha makombora cha China Qingdao, wakiondoka kwenda kufanya mazoezi ya kijeshi katika Bahari ya China Mashariki.
Wahudumu wa chombo cha kurusha makombora cha China Qingdao, wakiondoka kwenda kufanya mazoezi ya kijeshi katika Bahari ya China Mashariki. AP
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Taiwan Tsai Ing-wen amesema Jumatano kwamba kisiwa hicho "hakitarudi nyuma" kutokana na tishio kutoka China, ambayo inajiandaa kufanya luteka ya kijeshi karibu na pwani ya Taiwan kulipiza kisasi kwa ziara ya Nancy Pelosi.

Wizara ya Ulinzi ya China imeahidi "jeshi litachukuwa hatua kali", na mfululizo wa mazoezi ya kijeshi yatakayokizingira kisiwa hicho kuanzia siku ya Alhamisi, ikiwa ni pamoja na "kurusha makombora ya masafa marefu" katika Mlango wa Taiwan, unaotenganisha kisiwa hicho katika China Bara.

Mazoezi haya "yanachukua hatua muhimu na halali ili kujibu chokochoko kali za baadhi ya wanasiasa wa Marekani na watu wanaotaka kujitenga wa Taiwan", msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, Hua Chunying, ameviambia vyombo vya habari.

"Vitisho vikali"

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na jeshi la China, sehemu ya operesheni za kijeshi zitafanyika kilomita 20 kutoka pwani ya Taiwan. Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Taiwan, Sun Li-fang, amesema: "Baadhi ya maeneo ya uendeshaji ya China yanaingilia ... maji ya eneo la Taiwan."Β 

Baraza la Masuala ya Bara, chombo kinachoweka wazi sera ya serikali ya Taiwan dhidi ya Beijing, limeshutumu utawala wa China kwa kufanya "uonevu mbaya" ambao "utaathiri pakubwa amani na ustawi wa Asia Mashariki yote". Wakati huo huo Japan imesema "inatiwa wasiwasi" na mazoezi ya China, ikisema kuwa baadhi ya mazoezi hayo yataingilia ukanda wake mahsusi wa kiuchumi au Exclusive Economic Zone, (EEZ).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.