Pata taarifa kuu

Japan: Tuna wasiwasi na tangazo la mazoezi ya kijeshi ya China katika Mlango wa Taiwan

Japan imesema kuwa ina wasiwasi mkubwa baada ya China kutangaza kuwa inaansa luteka za kijeshi wakati Spika wa Bunge la Marekani Nancy Pelosi akikitembelea kisiwa cha Taiwan.

Nancy Pelosi, Spika wa Bunge la Wawakilishi la Marekani akiwasili Taiwan.
Nancy Pelosi, Spika wa Bunge la Wawakilishi la Marekani akiwasili Taiwan. © 路透社图片
Matangazo ya kibiashara

Jeshi la  China litafanya mazoezi makali karibu na kisiwa cha Taiwan kuanzia tarehe 4 hadi 7 Agosti kujibu ziara ya Spika wa Bunge la Wawakilishi la Marekani, Nancy Pelosi, nchini Taiwan, ambako aliwasili Jumanne jeshi limesema katika taarifa.

Mazoezi ya kijeshi ya China yatajumuisha "ufyatuaji risasi wa masafa marefu kwenye Mlango wa Bahari wa Taiwan," kulingana na jeshi.

"Hatua hii inaelekezwa kujibu ongezeko la hivi karibuni  la kushtua la Marekani kuhusu suala la Taiwan," msemaji wa kijeshi alisema katika taarifa.

Pia alihakikisha kwamba "ni onyo kubwa kwa majeshi ya uhuru wa Taiwan au kwa wale wanaotafuta uhuru."

Beijing inadai kisiwa hicho kama eneo lake na imechukua safari ya kiongozi huyo wa bunge, ambaye pia ni afisa wa ngazi ya juu zaidi wa Marekani kisiwani  Taiwan katika miaka 25, kama dharau kubwa.

Awali China ilitahadharisha kuwa Marekani italipa gharama ikiwa Spika wa Bunge Nancy Pelosi atazuru Taiwan. Wakati huo huo Urusi imesema imefungamana na China, na kuita ziara ya Pelosi kuwa uchokozi mtupu.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa China Hua Chunying amesema katika mkutano wa kawaida na waandishi habari kwamba upande wa Marekani utabeba dhamana na kulipa gharama ya kudhoofisha maslahi ya usalama ya China.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.