Pelosi aitaka China kutokuwa na wasiwasi wowote kuhusiana na ziara yake Taiwan
Spika wa bunge la Marekani Nancy Pelosi, amekutana na rais wa Taiwan, Tsai Ing-wen ambapo kabla ya hapo, allihotubia bunge na kusisitiza kuwa ziara yake ni ya kuimarisha urafiki kati ya nchi hizo mbili.
Imechapishwa:
Pelosi ameipongeza Taiwan kwa kuwa nchi huru duniani na kwamba anajisikia vizuri kuitwa rafiki wa Taiwan.
Aidha, amesema , ziara yake inalenga kutafuta namna ya nchi yake inavyoweza kuimarisha usalama na Taiwan ,kuinua uchumi na kuboresha ushirikiano wa mabunge yote mawili.
Baada ya hotuba hiyo ,spika Pelosi amekutana na rais Tsai Ing- Wen ambaye amempa zawadi ya medali maalum ya kutambua juhudi zake kuongeza mawasiliano kati ya Washington na Taipei.
Ziara ya Pelosi imekosolewa na China ,iliyokuwa imetoa onyo kali kwa Taiwan iwapo itampokea kiongozi huyo wa juu wa Marekani. China inaendelea kusisitiza, Taiwan ni sehemu ya nchi yake na sio huru.