Pata taarifa kuu

Washington yataka ulimwengu kuunga mkono ushiriki wa Taiwan katika taasisi za UN

Kauli hiyo ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani inakuja huku kukiwa na mvutano kati yake na China, hasa kuhusu kisiwa hicho kinachodaiwa na Beijing kuwa ni sehemu ya ardhi yake.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Anthony Blinken Februari 4, 2021 mjini Washington.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Anthony Blinken Februari 4, 2021 mjini Washington. AP - Evan Vucci
Matangazo ya kibiashara

Anthony Blinken amezungumza siku moja baada ya maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka hamsini ya China ya Kikomunisti kuingia Umoja wa Mataifa, kuchukua nafasi ya Taiwan. Katika taarifa hiyo, waziri wa mambo ya nje wa Marekani amebaini kwamba Taiwan ni mafanikio ya kidemokrasia na kwamba kutengwa kwake kunadhoofisha kazi muhimu ya Umoja wa Mataifa na mashirika yake.

Hili huenda likaichukiza sana Beijing, kwani serikali ya kikomunisti inadai mamlaka juu ya kisiwa hicho na imeendelea kutangaza hilo. Mapema mwezi huu, katika kuadhimisha kumbukumbu ya China ya Kikomunisti, idadi kubwa ya ndege za kijeshi za China ziliingia katika eneo la ulinzi wa anga la Taiwan katika siku chache.

Hofu ya migogoro ya silaha

Hofu ya kudhibiti kisiwa hicho kwa nguvu inazidi kuongezeka. Miongoni mwa mivutano yote kati ya China na Marekani, suala la Taiwan ndilo pekee linalofikiriwa kuwa linaweza kuzua mzozo wa silaha.

Wiki iliyopita, China pia ilimtaka rais wa Marekani kuwa makini baada ya Joe Biden kueleza kuwa Marekani itaingilia kati shambulio la China na kwamba kuna dhamira ya kufanya hivyo. Ilionekana kama mageuzi ya mafundisho ya kihistoria ya utata wa kimkakati, na utawala wa Marekani ulikuwa mwepesi kueleza kwamba hakuna kilichobadilika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.