Pata taarifa kuu
TAIWAN-USALAMA

Vita vya maneno vyaendelea kati ya Marekani na China kuhusu Taiwan

Rais wa Taiwan, Tsai Ing-wen, amesema ana imani kuwa Marekani itailinda iwapo, China itaamua kuishambulia kijeshi.

Rais Tsai Ing-wen: 'Tuna ushirikiano mpana na Marekani unaolenga kuongeza uwezo wetu wa ulinzi'
Rais Tsai Ing-wen: 'Tuna ushirikiano mpana na Marekani unaolenga kuongeza uwezo wetu wa ulinzi' Sam Yeh AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Katika mahojiano na Televisheni ya Marekani CNN, rais huyo hatua ya Marekani kutuma wanajeshi wake kuwapa mafunzo wale wa Taiwan inaleta matumaini makubwa.

China imekuwa ikisema eneo la Taiwan ni ardhi yake, na hivi karibuni ndege zake za kivita zilionekana zikipaa juu ya anga ya kisiwa hicho, huku ikionya Marekani kuhusu kuingilia masuala ya ndani ya nchi yake.

Siku ya Jumanne wiki hii Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani aliomba "ushiriki mkubwa" wa Taiwan katika Umoja wa Mataifa, pendekezo lisilokubalika kwa Beijing ambayo inakichukulia kisiwa hicho kama moja ya majimbo yake, shirika la habari la AFP limesema.

Anthony Blinken alizungumza siku moja baada ya maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka hamsini ya China ya Kikomunisti kuingia Umoja wa Mataifa, kuchukua nafasi ya Taiwan.

Katika taarifa hiyo, waziri wa mambo ya nje wa Marekani alibaini kwamba Taiwan ni mafanikio ya kidemokrasia na kwamba kutengwa kwake kunadhoofisha kazi muhimu ya Umoja wa Mataifa na mashirika yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.