Pata taarifa kuu
CHINA-USHIRIKIANO

Beijing yamjibu Blinken kuhusaiana na ushiriki wa Taiwan katika Umoja wa Mataifa

Taiwan "haina haki" ya kushiriki katika Umoja wa Mataifa, Beijing imesema Jumatano, Oktoba 27, ikikataa pendekezo la Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken.

Makombora ya Dong Feng 17 yaliyozinduliwa na Beijing kwenye eneola Tiananmen Square katika maadhimisho ya miaka 70 ya kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China, Oktoba 1, 2019.
Makombora ya Dong Feng 17 yaliyozinduliwa na Beijing kwenye eneola Tiananmen Square katika maadhimisho ya miaka 70 ya kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China, Oktoba 1, 2019. AP - Ng Han Guan
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani aliomba Jumanne "ushiriki mkubwa" wa Taiwan katika Umoja wa Mataifa, pendekezo lisilokubalika kwa Beijing ambayo inakichukulia kisiwa hicho kama moja ya majimbo yake, shirika la habari la AFP limesema.

Anthony Blinken alizungumza siku moja baada ya maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka hamsini ya China ya Kikomunisti kuingia Umoja wa Mataifa, kuchukua nafasi ya Taiwan.

Katika taarifa hiyo, waziri wa mambo ya nje wa Marekani alibaini kwamba Taiwan ni mafanikio ya kidemokrasia na kwamba kutengwa kwake kunadhoofisha kazi muhimu ya Umoja wa Mataifa na mashirika yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.