Pata taarifa kuu
INDIA-CHINA-USALAMA

Modi ahubiri umoja nchini India baada ya makabiliano na China

Waziri Mkuu wa India amekutana na vyama vinavyowakilishwa bungeni kwa mazungumzo kuhusu mgogoro wa eneo la mpakani na China. Makabiliano kwenye mpaka wa Himalaya yalisababisha vifo vya wanajeshi 20 wa India na 5 kutoka China.

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi wakati wa mkutano na viongozi wa vyama vikuu nchini India kupitia video, Juni 20, 2020 huko New Delhi.
Waziri Mkuu wa India Narendra Modi wakati wa mkutano na viongozi wa vyama vikuu nchini India kupitia video, Juni 20, 2020 huko New Delhi. Handout / PIB / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo idadi kubwa ya askari imepelekwa kwenye eneo hilo la mpakani lenye utata.

"Wachina hawajaingia katika ardhi yetu na hawajadhibiti kituo chochote cha jeshi. Ni kwa maneno hayo, Waziri Mkuu wa India alihitimisha mkutano na wajumbe wa vyama vinavyowakilishwa bungeni kupitia video. Wengi wao wamemuunga mkono Narendra Modi katika azimio lake la kutafuta amani akiwa bado tayari kupambana na China.

Lakini wengine wanahoji jinsi ya kutatua mgogoro huo ambao umedumu sasa zaidi ya mwezi mmoja: "Kwanini viongozi wa kisiasa wa India hawakuanza kujadili na wenzao wa China tangu makabiliano ya kwanza ya Mei 5", amehoji Sonia Gandhi, spika wa Bunge kutoka chama kikuu cha upinzani katika Bunge la India.

Aam Admi, kiongozi wa serikali ya jimbo la Delhi, amehoji kwa nini kulikuwa na makabiliano ikiwa askari wa China hawakuingia katika ardhji ya India.

Kwa sasa, New Delhi imepeleka ndege nyingi za kivita na helikopta kwenye eneo hilo la mpakani. Na chjina imefanya hivyo kwa upande wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.