Pata taarifa kuu
INDIA-CHINA-USALAMA

Sintofahamu yaendelea kati ya China na India baada ya makabiliano

Mapigano kati ya majeshi ya India na China yamegramu vifo vya askari 20 wa India na upande wa China kunaripotiwa vifo au majeruhi 40, kulingana na vyanzo kutoka India. Hali ya sintofahamu imeendelea katika jimbo Ladakh.

Waandamanaji nchini India wakichoma picha ya Rais wa China Xi Jinping, Juni 16, 2020 huko Ahmedabad.
Waandamanaji nchini India wakichoma picha ya Rais wa China Xi Jinping, Juni 16, 2020 huko Ahmedabad. REUTERS/Amit Dave
Matangazo ya kibiashara

Makabiliano makali yalitokea Jumatatu wiki hii kati ya jeshi la India na lile la China kwenye mpaka wao wenye utata wa Ladakh, kwenye Mlima wa Himalaya.

Hali hii inaonesha mzozo mkubwa kabisa kuwahi kutokea tangu miaka 45 iliyopita. Mvutano huu umeendelea kwa miezi miwili sasa kati ya nchi hizi mbili zenye nguvu ya kinyuklia kwenye eneo hilo la mpakani, lakini hii inaonesha jinsi gani mzozo huu umechukuwa sura nyingine.

Makabiliano haya yalitokea katika bonde la Galwan, moja wapo ya maeneo mawili ya mipakani yenye utata kati ya majeshi ya China na yale ya India kwa zaidi ya mwezi mmoja huko Ladakh.

Kinachoshangaza ni kwamba majeshi hayo kutoka nchi hizo mbili yalikuwa yameanza kujiondoa kwenye bonde la Galwan wiki iliyopita.

Na Jumatatu hii, Juni 15, wawakilishi kutoka pande hizo mbili walitarajiwa kukutana ili kuendelea kujadili kuhusu ongezeko la hali hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.