Pata taarifa kuu
INDIA-CHINA-USALAMA

Waziri Mkuu wa India aapa kulipiza kisasi dhidi ya China

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi amesema kuuawa kwa wanajeshi wake 20 baada ya mapigano na wanajeshi wa China katika eneo la mpaka lenye mgogoro la Himalayan, hakutaenda bure.

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi.
Waziri Mkuu wa India Narendra Modi. PRAKASH SINGH / AFP
Matangazo ya kibiashara

Modi amewaambia raia wa India kuwa, nchi hiyo inajivunia wanajeshi wake kuuawa wakati wanapigana na wanajesehi wa China katika eneo hilo lenye utata.

Ripoti zinasema wanajeshi hao walipigana kwa kutumia fimbo zilizokuwa na misumari.

Nchi zote mbili zimelaumiana baada ya kutokea kwa mapiganano haya na tayari zimeanzisha mazungumzo kutatua sintofahamu inayoshuhudiwa.

Hii ndio mara ya kwanza wanajeshi wa nchi hizo mbili wanapigana katika eneo la Jimbo lenye utata la Kashmir baada ya miaka 45.

Kuna wasiwasi kuwa, kuna baadhi ya wanajeshi wa India ambao hawajapatikana baada ya vita hivyo, huku ikiaminiwa kuwa China pia imewapoteza wanajeshi wake, lakini Beijing haijasema lolote.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.