Pata taarifa kuu
CHINA-INDIA-USALAMA

China na India zakubaliana kutuliza uhasama kwenye eneo la mpakani

China na India zimichukua uamuzi wa kutuliza machafuko katika mpaka wa Himalaya wanaozozania, siku chache baada ya machafuko yaliyosababisha vifo kadhaa kati ya majeshi ya pande hizo mbili.

Ni katika eneo hili la mlima mrefu wa Himalaya, ambapo kulitokea machafuko kati ya vikosi vya ulizi vya China na India.
Ni katika eneo hili la mlima mrefu wa Himalaya, ambapo kulitokea machafuko kati ya vikosi vya ulizi vya China na India. AFP/Tauseef Mustafa
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na shirika la habari la AFP likinukuu duru za kuaminika, mazungumzo kati ya Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi na mwenzake wa Mambo ya Nje wa India Subrahmanyam Jaishankarhayo yamefanyika kwa njia ya simu wakati India inawapeleka maafisa wake wa kukabiliana na fujo katika eneo hilo Himalaya nyuma ya Tibet, huku kituo cha televisheni cha serikali ya China CCTV, kikionyesha kanda ya video ya majeshi ya China yakifanya luteka katika eneo hilo la Tibet.

Siku ya Alhamisi Waziri Mkuu wa India Narendra Modi amlisema kuuawa kwa wanajeshi wake 20 baada ya mapigano na wanajeshi wa China katika eneo la mpaka lenye mgogoro la Himalayan, hakutaenda bure.

Modi aliwaambia raia wa India kuwa, nchi hiyo inajivunia wanajeshi wake kuuawa wakati wanapigana na wanajesehi wa China katika eneo hilo lenye utata.

Ripoti zinasema wanajeshi hao walipigana kwa kutumia fimbo zilizokuwa na misumari.

Nchi zote mbili zimelaumiana baada ya kutokea kwa mapiganano hayo.

Hii ndio mara ya kwanza wanajeshi wa nchi hizo mbili wanapigana katika eneo la Jimbo lenye utata la Kashmir baada ya miaka 45.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.