Pata taarifa kuu
INDIA-CHINA-USALAMA

Wanajeshi watatu wa India wauawa katika mkoa wenye utata wa Ladakh

Makabiliano makali yametokea Jumatatu wiki hii kati ya jeshi la India na lile la China kwenye mpaka wao wenye utata wa Ladakh, kwenye Mlima wa Himalaya.

Ziwa la Pangong ambalo hutenganisha India na China.
Ziwa la Pangong ambalo hutenganisha India na China. Prakash SINGH / AFP
Matangazo ya kibiashara

Wanajeshi watatu wa India na watano kutoka China wameripotiwa kuuawa, na wengine kadhaa wamejeruhiwa vibaya. Hali hii inaonesha mzozo mkubwa kabisa kuwahi kutokea tangu miaka 45 iliyopita. Mvutano huu umeendelea kwa miezi miwili sasa kati ya nchi hizi mbili zenye nguvu ya kinyuklia kwenye eneo hilo la mpakani, lakini hii inaonesha jinsi gani mzozo huu umechukuwa sura nyingine.

Makabiliano haya yametokea katika bonde la Galwan, moja wapo ya maeneo mawili ya mipakani yenye utata kati ya majeshi ya China na yale ya India kwa zaidi ya mwezi mmoja huko Ladakh. Kinachoshangaza ni kwamba majeshi hayo kutoka nchi hizo mbili yalikuwa yameanza kujiondoa kwene bonde la Galwan wiki iliyopita.

Na Jumatatu hii, Juni 15, wawakilishi kutoka pande hizo mbili walitarajiwa kukutana ili kuendelea kujadili kuhusu ongezeko la hali hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.