Pata taarifa kuu
UTAFUTAJI-AJALI

Nyambizi ya 'Titan' iliyopotea: 'Sehemu ya mabaki' yapatikana karibu na 'Titanic'

'Sehemu ya mabaki' imegunduliwa katika Bahari ya Atlantiki karibu na mabaki ya mli kubwa ya Titanic na roboti inayoshiriki katika utafiti wa kimataifa ili kupata meli ya kitalii ya kisayansi ambayo ilitoweka tangu Jumapili.

Picha hii isiyo na tarehe, ya OceanGate Expeditions, inaonyesha uzinduzi wa nyambizi yao ya Titan kutoka kwenye jukwaa.
Picha hii isiyo na tarehe, ya OceanGate Expeditions, inaonyesha uzinduzi wa nyambizi yao ya Titan kutoka kwenye jukwaa. AFP - HANDOUT
Matangazo ya kibiashara

Walinzi wa Pwani wa Marekani wametangaza kwenye Twitter siku ya Alhamisi kwamba 'mabaki' yamegunduliwa na ROV 'katika eneo la utafutaji [Remotely Operated Vehicle, au gari Linaloendeshwa kwa umbali] karibu na mabaki ya meli kubwa ya Titanic',  meli maarufu iliyozama miaka 111 iliyopita kwenye pwani ya Marekani na Canada.

'Wataalamu wanachunguza habari hii' ambayo itajadiliwa wakati wa mkutano na waandishi wa habari huko Boston (kaskazini-mashariki) saa tisa kamili alaasiri saa za Marekani (sawa na saa tano usiku za za Afrika Mshariki), kulingana na walinzi wa pwani, ambao wanasimamia zoezi la utafutaji na uokoaji ambalo halijawahi kufanywa ili kupata abiria watano wakiwa hai katika nyambizi hii ndogo , Titan, iliyotoweka tangu siku sita zilizopita: raia wawili wenye urais pacha wa Pakistani na Uingereza, Muingerezammoja, Mfaransa mmoja na Marekani mmoja.

Admirali John Mauger anayeongoza utafutaji huopamoja na na kamanda Jamie Frederick watazungumza katika kikao hicho.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.