Pata taarifa kuu

Nyambizi ya 'Titan': Utafutaji washika kasi, wasiwasi watanda juu ya akiba ya oksijeni

Shughuli za kutafuta nyambizi ndogo ya kitalii iliyopotea hivi karibuni katika maji yanayounganisha Canada na Marekani zinashika kasi ili kujaribu kupata nyambizi hiyo 'Titan'. Kwa bahati mbaya, akiba ya oksijeni ya nyambizi hiyo itaisha hivi karibuni.

Zoezi la kutafuta meli ndogo ya kitalii iliyopotea majini yashik kasi ili kujaribu kupata Titan inayoweza kuzama (picha yetu).
Zoezi la kutafuta meli ndogo ya kitalii iliyopotea majini yashik kasi ili kujaribu kupata Titan inayoweza kuzama (picha yetu). via REUTERS - OCEANGATE EXPEDITIONS
Matangazo ya kibiashara

Nyambizi hii ya kitalii iliondoka na saa 96 ya hifadhi ya hewa ya kupumua, lakini muda wa hifadhi ya oksijeni hiyo hutegemea mambo mengi kuanzia hali ya nyambizi, hali ya kimwili na hata ya akili ya watu waliomo katika nyambizi hiyo.

Nahodha wa kikosi cha walinzi wa Pwani ya Marekani anaendelea kuonyesha matumaini yake, lakini wengi wameanza kukata tamaa. Kelele ambazo zimegunduliwa katika eneo hilo hadi sasa hazijatoa chochote.

Eneo la utafutaji ndani ya maji linachukua kilomita za mraba 20,000. 

Shughuli ngumu

Meli ya utafiti ya Ifremer ya Ufaransa iliyokuwa na roboti inayoweza kuruka hadi kwenye mabaki ya meli kubwa ya Titanic iliwasili usiku. Meli hiyo Victor 6000 ina mikono miwili ya kimakanika inayoweza kufanya kazi ngumu, kama vile kukata au kuondoa mabaki.

Lakini hata kama Titan ilipatikana haraka, wataalam wanakadiria kuwa itachukua masaa kadhaa kuileta nchi kavu na kuwatoa watu ambao wamekwama katika meli hiyo, hasa ikiwa iko chini ya bahari, ambapo shinikizo ni kubwa na giza kamili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.