Pata taarifa kuu

Haiti: Antony Blinken anaomba uingiliaji kati wa kijeshi, ambao Canada haitaki kusimamia

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Anthony Blinken, ambaye yuko ziarani nchini Canada hadi Ijumaa hii jioni, amezungumza kwa kirefu na mwenzake wa Canada Mélanie Joly kuhusu mzozo ambao Haiti inapitia kwa sasa. 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken, na Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada, Mélanie Joly, katika mkutano na waandishi wa habari, Alhamisi, Oktoba 27.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken, na Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada, Mélanie Joly, katika mkutano na waandishi wa habari, Alhamisi, Oktoba 27. AP - Sean Kilpatrick
Matangazo ya kibiashara

Hata kabla ya kuwasili kwake Ottawa, Marekani ilikuwa imedokeza kwamba mamlaka ya Canada inaweza kuongoza kikosi cha kimataifa cha kuingilia kati. Pendekezo ambalo Canada inaonekana kupinga.

Kwa sasa, Canada haina haraka ya kuingilia kijeshi nchini Haiti, licha ya msisitizo wa nchi jirani ya Marekani. Katika mkutano na waandishi wa habari pamoja na mwenzake wa Marekani, Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada, amebaini kwamba suluhisho la mgogoro huu lazima lipitie kwa raia wa Haiti.

"Hakutakuwa na uamuzi ambao utafanywa bila kuwashirikisha Wahaiti. Nimekuwa nikisema kila mara kuwa itakuwa kwa niaba ya ya Wahaiti kwa sababu, ni kwa manufaa yao. Kwa sababu sasa hivi, raia ndio wanaoteseka nchini Haiti. Kwa hiyo lengo letu ni kuwasaidia,” amesema Mélanie Joly.

Ujumbe wa Canada kwa sasa unashauriana na washikadau  ili "kuchunguza njia tofauti za kuwasaidia raia wa Haiti", ilisema serikali, ambayo inapanga kuunga mkono "suluhisho lililopendekezwa na Wahaiti ili kurejesha ufikiaji wa bidhaa na huduma muhimu".

Timu ya Canada pia iko uwanjani ili kutathmini uwezo ambao erikali ya Haiti itatumia kuondoa vizuizi vya barabarani, na kuwezesha polisi kufanya kazi yao. Waziri wa Mambo ya Nje anasubiri sasisho hili ili kujua ni bunduki gani zinahitajika ili kusaidia kweli Haiti.

Ziara hiyo inakuja wakati jumuiya ya kimataifa inachunguza jinsi ya kuongeza misaada yake kwa Haiti, ambayo imetoa wito wa kusaidiwa kutokana na kuzorota kwa hali ya kibinadamu na usalama, ikiwa ni pamoja na kupitia kikosi cha kulinda amani. Wito wa serikali ya Haiti umetolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres.

Lakini wazo hili la jeshi haliungwi mkono na wengi, hata raia wa Ukraine na ndani ya Baraza la Usalama hawaungi mkono, na hakuna nchi ambayo bado imejitolea kuliongoza. Marekani imebaini kwamba iko tayari kuunga mkono jeshi la aina hiyo lakini sio kuliongoza na huo ndio msimamo wa Ufaransa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.