Pata taarifa kuu

Haiti: Mvutano unaendelea kuongezeka baada ya maandamano mapya na makabiliano

Maandamano ya kupinga kupanda kwa bei ya mafuta na gharama ya maisha yamefanyika katika mitaa ya Haiti siku ya Jumatano (tarehe 28 Septemba). Maelfu ya watu walimiminika mitaani huko Gonaives, Cap Haitien au Port-au-Prince ambao pia walitaka Waziri Mkuu Ariel Henri ajiuzulu. Hali ya taharuki inaendelea kuongezeka nchini humo na kusababisha makabiliano na polisi.

Mmoja wa waandamanaji anayetaka Waziri Mkuu Ariel Henry ajiuzulu akiitika mgomo katika ngazi ya kitaifa huko Port-au-Prince mnamo Septemba 28.
Mmoja wa waandamanaji anayetaka Waziri Mkuu Ariel Henry ajiuzulu akiitika mgomo katika ngazi ya kitaifa huko Port-au-Prince mnamo Septemba 28. © Richard Pierrin / AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika mji wa Gonaïves, kaskazini mwa nchi, "vizuizi vilivyowashwa moto na vipande vya chupa vinaupa mji huo sura ya jiji lililozingirwa na vita," Gazeti la Nouvelliste limebaini. "Kiongozi wa zamani wa waasi wa kundi la 2004 dhidi ya Rais wa zamani Jean Bertrand Aristide, Wilfort Ferdinand anayejulikana kwa jina maarufu la Ti Will, aliongoza maandamano hayo," linabainisha Gazeti la Haiti. Gazeti hilo linazungumzia maandamano ya "amani", lakini yanatishia: ikiwa Waziri Mkuu Ariel Henri "atakataa kuondoka, eneo la kaskazini litajitenga na nchi nzima na tutafanya hivyo kijeshi kwa kuwaita askari wote wa zamani wa kundi la zamani la waasi la 2004. ".

Pia Kaskazini, katika mkoa wa Cap Haitien, waandamanaji waliandamana kwa mpango wa chama cha Pitit Desalin, ambacho kiongozi wake pia alimtaka Waziri Mkuu ajiuzulu. “Mwishoni mwa maandamano haya, waandamanaji waliharibu duka kuu katika mji huo,” limeripoti Gazeti la Le Nouvelliste. Hatimaye kwenye barabara kuu ya Delmas, karibu na Port-au-Prince, "umati mkubwa uliingia kwenye barabara kuu ya Delmas", na kuweka vizuizi vinavyowaka moto, anasema RezoNodwès. Watu kadhaa wameripotiwa kujeruhiwa na risasi za polisi.

Wakati huo huo, hakuna neno kutoka kwa upande wa serikali. Gazeti la Le Nouvelliste linabainisha kwamba "kipimo cha mwisho au uelewa wa hali hiyo ulitolewa na Kansela Jean-Victor Généus, ambaye kwa ujumla, 'amesema 'hali iko chini ya udhibiti''". Matamshi yaliyotolewa siku ya Jumatatu, na yalikosolewa wakati wa maandamano, ambayo yataendelea, kwa sababu ikiwa kulingana na Gazeti la Haiti wanaharakati wa vyama vya wafanyakazi wamesitisha mgomo, "wanatoa wito kwa watu kuandamana leo na kesho dhidi ya serikali".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.